33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Bodi ya Mikopo yatoa siku 60 kwa wadeni wake

HESLB Ag ED Jerry SabiNa Mwandishi Wetu,Dar

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imetoa siku 60 kuanzia leo kwa wanufaika wote wa mikopo wanaodaiwa kujitokeza kulipa madeni yao kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji  wa bodi hiyo Dar es Salaam jana, Jerry Sabi  ilisema waajiri wanatakiwa kutekeleza wajibu wao wa kisheria wa kuwasilisha taarifa za waajiriwa wao waliohitimu vyuo vya elimu ya juu ndani na nje ya nchi ndani ya kipindi hicho, majina kamili ya waajiriwa, vyuo na mwaka waliohitimu.

Taarifa hiyo, ilisema sheria iliyoanzisha HESLB inatoa wajibu kwa mnufaika wa mikopo ya elimu ya juu na pia wajibu kwa mwajiri.

“Taarifa hii inalenga kuwakumbusha waajiri ambao hawatimizi wajibu wao kisheria (kifungu cha 20) wa kuwasilisha majina ya waajiriwa wao wote ambao ni wahitimu wa vyuo vikuu kwa HESLB ndani ya siku 28 tangu waajiriwe, adhabu ya kutotekeleza wajibu huo kwa mwajiri ni faini ya Sh milioni 7 au kifungo au vyote kwa pamoja,” ilisema.

Taarifa hiyo, ilisema baada ya HESLB kupokea orodha kutoka kwa mwajiri, itafanya uchambuzi ili kubaini wanufaika na kumwelekeza mwajiri namna ya kuingiza makato ya marejesho kwenye mshahara wa mnufaika na kuwasilisha kwenye bodi.

“Adhabu ya kutowasilisha makato kwenye bodi ni faini ya asilimia 10 ya makato yote ambayo hayajawasilishwa na faini hii inapaswa kulipwa na mwajiri,”ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo, iliongeza kuwa kama mnufaika wa mkopo atashindwa kutoa taarifa hizo, atashtakiwa mahakamani.

“Bodi inapenda kuwakumbusha wazazi, walezi na wadhamini wa wanafunzi walionufaika na mikopo kuwa wana wajibu wa kisheria (chini ya kifungu cha 22 cha sheria ya HESLB) wa kuhakikisha taarifa muhimu za mnufaika waliyemdhamini zinaifikia bodi mapema,”ilisema taarifa hiyo.

Bodi hiyo, ilianzishwa kwa sheria ya Bunge na 9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi Julai, 2005 ili pamoja na majukumu mengine kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles