27.7 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

CHADEMA WALALAMIKIA VIONGOZI WAO KUPORWA MASHAMBA

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

UONGOZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Kati, umelalamikia kitendo cha Serikali kuchukua mashamba ya viongzi wa chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kati, Alphonce Mbasa, alisema kitendo cha wanachama wao kuporwa mali zao au kuharibiwa mali zao, kinaweza kujenga chuki na kudidimiza siasa za upinzani.

“Tumekuwa tukishuhudia mara kwa mara viongozi wa Chadema wakiporwa mali zao au kuharibiwa mali walizonazo, huku baadhi ya viongozi wa chama tawala wakiwa wanamiliki mali kama hizo, lakini hakuna hatua yoyote ambayo inafanyika juu yao.

“Hivi karibuni Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, alifanyiwa ‘figisu’ katika jengo la Bilcanas, kisha akafanyiwa hivyo katika shamba lake la maua huko wilayani Hai, Kilimanjaro.

“Kama hiyo haitoshi, tumeona Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Fredrick Sumaye, akiporwa mashamba yake kwa madai kuwa hayajaendelezwa.

“Mbali na Sumaye, hata mke wake naye ameporwa shamba kwa madai ya kutoliendeleza. Je, kwanini mambo hayo yanafanywa kwa viongozi wa Chadema na viongozi wa CCM hawaguswi?

“Kwa hiyo, tunaitaka Serikali kutochukua uamuzi wa kuwakomoa wanasiasa wa upinzani kwa kuwa vyama vya siasa vya upinzani vipo kwa mujibu wa sheria ya vyama vingi,” alisema Mbassa.

“Kama kweli operesheni hii ina nia njema, basi hata mashamba ya marais wastaafu yachukuliwe kwa sababu baadhi hayajaendelezwa,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Siasa za Tanzania sasa zimefika mahali pabaya. Ni siasa za chuki, kukomoana, kulipana visasi na mambo mengine mengi. Amani inaonekana kupotea. Sitashangaa kama vurugu zikitokea katika nchi yetu ambayo ilikuwa ni kisiwa cha amani. Ni aibu kwa nchi yetu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles