29.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 4, 2023

Contact us: [email protected]

AUAWA KWA RISASI AKIJARIBU KUIBA BENKI NBC

NA TIMOTHY ITEMBE

MTU Mmoja ambaye jina lake halikufahamika anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 30-35 ameuawa kwa risasi na polisi baada ya kuingia katika benki ya NBC usiku.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime na Rorya, Henry Mwaibambe,  alisema  mtu huyo aliingia ndani ya benki ya NBC kwa kupitia kwenye tundu lililoko karibu na ATM.

Alisema  Agosti 19, mwaka huu saa 6:04 usiku  mtu huyo ambaye hajafahamika jina wala  makazi yake alifariki dunia baada ya kujeruhiwa kwa risasi na  polisi waliokuwa kwenye lindo katika benki hiyo baada ya kumtaka kujisalimisha na kukaidi amri hiyo.

“Mtu huyo  alifanya matukio mawili ya kushangaza kwa siku tofauti katika benki hiyo.

“Tukio la kwanza Agosti 18, mwaka huu kati ya saa 4.00 na 6.00 usiku aliingia na kufanikiwa kutoka ndani ya benki  bila kuonekana na hakuchukua  chochote.

“Tukio la siku ya pili Agosti 19, mwaka huu saa 6:04 usiku aliingia na askari waliokuwa katika  lindo waligundua wakati king’ora cha benki kikipiga kelele.

“Baada ya kelele askari walimtaka mtu huyo kujisalimisha lakini  alikaidi na kuanza kukimbia.

“Polisi walifyatua risasi ya hewani kumtishia lakini hakusimama walifyatua risasi ya pili ambayo ilimpata na kumjeruhi mguuni na shingoni na kuanguka chini.

“Walimuchukua na kumkimbiza katika hospitali ya wilaya katika jitihada hizo marehemu alifariki akiwa  njiani kabla hajafikishwa  hospitalini,” alisema Mwaibambe.

Mwaibambe amewataka wakazi wote wa Tarime na Rorya kutoa taarifa  wanapokuwa na  shaka na mtu yeyote ambaye ana mazingira ya uhalifu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles