26.7 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

CHADEMA WAIOMBA SERIKALI IMSAKE BEN SAANANE

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana kuhusu kupotea kwa msaidizi wa mwenyekiti wa chama hicho, Ben Saanane. Kulia ni Ofi sa Habari, Tumaini Makene na Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana (Bavicha), Julius Mwita.
Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana kuhusu kupotea kwa msaidizi wa mwenyekiti wa chama hicho, Ben Saanane. Kulia ni Ofi sa Habari, Tumaini Makene na Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana (Bavicha), Julius Mwita.

Na ELIZABETH HOMBO-DAR ES SALAAM

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeitaka Serikali kutumia vyombo vyake vya ulinzi na usalama kumtafuta msaidizi wa mwenyekiti wa chama hicho, Bernard Saanane, ambaye ametoweka katika mazingira ya kutatanisha zaidi ya mwezi mmoja sasa.

Chadema imesema Serikali ndiyo yenye uwezo pekee wa kiufundi kujua na kuamuru mashirika ya simu kueleza mawasiliano yake ya mwisho yalivyokuwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema katika siku za karibuni, Saanane amekuwa akiongoza kampeni kwenye mitandao ya kijamii, kuhusu kuhakikiwa kwa shahada za uzamivu (PhD) kwa baadhi ya viongozi.

Mwanasheria huyo wa Chadema, alisema wakati fulani Saanane alitumiwa ujumbe wa maneno kupitia simu yake ya kiganjani akitishiwa kuacha kuikosoa Serikali.

“Nanukuu maneno aliyotumiwa: “Ben Saanane unachokitafuta ndani ya Serikali hii utakipata, kwa elimu na uwezo wako hatukutarajia ungefikia hatua ya ajabu kwa namna ulivyofikia, hujiulizi kwanini upo huru hadi muda huu.

“You are too young to die. Tunajua utaandika na hili, andika lakini the next post hutaandika ukiwa na uhuru wa kutosha, andika but your days are numbered.

“Unajua kuna rafiki yako alipuuza na hutaki kuandika kuhusu yeye, labda kwa kuwa alitangulia, andika Ben, andika sana, ongea,  sema lakini utajikuta mwenyewe na chatu,” alinukuu Lissu.

Alisema: “Katika miezi ya hivi karibuni watu ambao wamekuwa wakiikosoa Serikali kupitia mitandao ya kijamii wamekuwa wakikamatwa na watwambie kama wanamshikilia Ben Saanane ili tujue.

“Serikali ndiyo yenye udhibiti wa mipaka yetu kuanzia baharini, nchi kavu, mipaka yetu ya anga na hata katika bandari, hivyo ituambie,” alisema Lissu.

Aidha mbunge huyo wa Singida Mashariki alisema yeyote anayefahamu taarifa za Saanane azitoe hadharani katika vyombo vya habari, polisi na hata katika vyombo vingine vya Serikali.

Aidha Lissu alisema taarifa za kupotea kwa Saanane wamezifikisha ngazi za kimataifa na  wataendelea kuzisambaza ili dunia nzima ijue.

Akizungumzia kuhusu taarifa ambayo imesambaa katika mitandao ya kijamii kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe anajua aliko Saanane, alisema: “Mara ya mwisho Ben amewasiliana na mwenyekiti Novemba 14 mwaka huu akiwa Dodoma na huwa hawaongozani, bali Ben anafanyia kazi zake makao makuu ya chama.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles