FUNDI UJENZI KIZIMBANI AKITUHUMIWA KUBAKA

0
513

law-portal

ATUPENDA GEOFREY Na MANENO SELANYIKA-DAR ES SALAAM

FUNDI ujenzi na mkazi wa Mbezi Juu, Dar es Salaam, Said Juma (45), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, akituhumiwa kwa kosa la kumbaka msichana (jina tunalo) mwenye umri wa miaka 10.

Mbele ya Hakimu Issa Kasailo, Wakili wa Serikali, Matarasa Maharagande, alidai kwamba tukio hilo lilitokea Oktoba 18, mwaka huu maeneo ya Mbezi Juu, Wilaya ya Ubungo.

Wakili Matarasa alidai kwamba mtuhumiwa alimbaka msichana huyo na kumsababishia maumivu makali sehemu za siri na mwili mzima.

Mtuhumiwa alikana kutenda kosa hilo na wakili alidai kuwa upelelezi unaendelea.

Alirejeshwa rumande hadi Desemba 28, mwaka huu hadi kesi itakapotajwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here