27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

ALIYETOBOLEWA MACHO NA ‘SCORPION’ ATOA USHAHIDI

Wasamaria wema wakimsaidia shahidi namba moja na mlalamikaji, Said Mrisho aliyetobolewa macho, alipokwenda kutoa ushahidi Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam jana. PICHA NDOGO ni mtuhumiwa wa kesi hiyo, Salum Njwete ‘Scorpion’ akipelekwa mahakamani.
Wasamaria wema wakimsaidia shahidi namba moja na mlalamikaji, Said Mrisho aliyetobolewa macho, alipokwenda kutoa ushahidi Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam jana. PICHA NDOGO ni mtuhumiwa wa kesi hiyo, Salum Njwete ‘Scorpion’ akipelekwa mahakamani.

FARAJA MASINDE NA BRIGHITER MASAKI TSJ-DAR ES SALAAM

SAIDI Mrisho ambaye ni shahidi namba moja na mlalamikaji kwenye kesi inayomkabili, Salum Njwete(34) maarufu Scorpion, ameieleza Mahakama ya Wilaya ya Ilala Dar es Salaam namna alivyotobolewa macho.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Nassoro Katuga mbele ya Hakimu Mkazi Flora Haule, Mrisho alidai Septemba 6, mwaka huu saa nne usiku akiwa Tabata Segerea, baada ya kufunga ofisi alikwenda kituoni kusubiri usafiri wa kwenda nyumbani kwake Makuburi karibu na Ubungo.

Shahidi huyo ambaye ni kinyozi alidai wakati anasubiri usafiri kituoni hapo ilipita bajaji na kumwuliza anakwenda wapi, ambapo alimwambia anakwenda Ubungo.

Baada ya majibizano hayo, mwenye bajaji alidai anakwenda Buguruni, hivyo anaweza kumsogeza hadi Tabata Relini ili akapande magari ya Ubungo.

“Wakati nimeshapanda bajaji na tumeelewana anifikishe Tabata Relini, ghafla dereva huyo aliniomba apite njia ambayo ni fupi ya kutokezea Buguruni hapo ndiko nitakapopata magari ya Ubungo kwani mimi naishi Makuburi,” alisema Mrisho.

Alidai baada ya kufikishwa Buguruni aliona kuna idadi kubwa ya watu waliokuwa wakiuza vitoweo vya kuku ambapo alisogea eneo hilo na kutaka kununua kwa ajili ya familia yake.

“Kulikuwa kuna wafanyabiashara wengi wa kuku eneo la Buguruni kituo cha Kwamnyamani kama saa 4,40 usiku ambapo nilichagua sehemu moja na kuuliza bei niliambiwa kuku mmoja Sh 7,000,” alisema.

Mrisho alidai kuwa wakati anaendelea na manunuzi na kuongea na muuzaji aliona mtu amesimama upande wake wa kulia begani ambapo mtu huyo alianza kumwita.

“Aliniambia broo nina shida nami nilimgeukia na kumuuliza unashida gani kama una shida sema nakusikiliza kama naweza kukusaidia nikusaidie lakini mtu huyo hakujibu ambapo niliendelea na manunuzi’’alisema.

Shahidi huyo alidai wakati anaendelea na manunuzi alishikwa na hofu kwani alikuwa amevaa cheni ya silva na mfuko wa suruali yake ulikuwa na fedha zilizoonesha kutuna.

“Ghafla nilishtukia ninachomwa kisu katika bega langu la kushoto, nilipogeuka niliendelea kuchomwa nikaanza kupiga kelele ya mwizi lakini sikupata msaada kwani nilishangazwa kuona watu wananiangalia bila kunipa msaada.

“Yule jamaa alijibu hakuna mtu wa kukusaidia, nilichomwa visu vinne tumboni nikaanguka chini. Wakati huo kuna watu walikuwa wanamwita Scorpion kwamba tayari umeshauwa wakati huo anaendelea kunikagua mfukoni,’’ alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles