29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

CHADEMA WAILILIA TUME YA UCHAGUZI

 

Na ELIZABETH HOMBO -DAR ES SALAAM           |         


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), isogeze mbele tarehe ya uchaguzi katika kata tano zilizopo Tunduma mkoani Mbeya, mbili zilizopo Iringa na moja iliyopo mkoani Arusha.

Imeiomba NEC itoe fursa hiyo ili wagombea wenye haki ya kugombea wapewe nafasi kwa sababu zilifanyika ‘rafu’ na uonevu kwa wagombea wao kuenguliwa katika maeneo hayo.

Pia chama hicho kimesema tayari wameandika barua za malalamiko na kuzipeleka tume kwa sababu hawajaachia maeneo hayo, bali wamekata rufaa.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Chadema, Reginald Munisi, alisema hadi jana wagombea udiwani wao katika kata 18 wameenguliwa.

“Mambo ambayo tumeyapeleka tume, pamoja na rufaa tulizozipeleka tume ni yale ambayo si ya kawaida, ambayo tumeyaona hadi sasa na tumeitaka tume wayazingatie, hasa kwenye uenguaji.

“Tume itendee haki rufaa zote tulizopeleka ili wagombea waweze kurudi kufanya kampeni. Lakini la pili kwa maeneo matatu ambayo sasa ni jambo la kipekee kwa Tunduma; kata zote tano ambazo wagombea wetu walinyimwa fomu, tunaitaka tume ihahirishe ule uchaguzi na iitishe upya mchakato ili wote wenye haki ya kugombea waweze kugombea.

“Kwa upande wa Arusha; Kata ya Terati ambayo mgombea wetu alinyang’anywa fomu mbele ya msimamizi wa uchaguzi akawekwa chini ya ulinzi na akapelekwa polisi yeye ambaye amedhulumiwa fomu, tunaiomba tume irudie ule mchakato.

“Kwa upande wa Iringa; kata mbili ya Gangilonga na Kwakilosa ambako msimamizi msaidizi alikataa kupokea fomu za wagombea wetu, tunaitaka tume isitishe mchakato ule pia,” alisema Munisi.

Alisema katika hali ambayo si ya kawaida, mahakimu wamekuwa wakikataa kuwaapisha wagombea wao jambo lililowalazimu kwenda kuapa nje ya wilaya zao.

Munisi alisema kuna baadhi ya maeneo rufaa zao zimekuwa zikikataliwa na kwamba Ubungo walipokea hivi karibuni, awali wahusika walikuwa wakiwakwepa.

Akizungumzia mchakato wa uchaguzi Jimbo la Buyungu mkoani Kigoma, alisema tayari mgombea wao amerudisha fomu na hakukuwa na uenguaji.

Alilitahadharisha Jeshi Polisi kufanya kazi zao na kamw

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles