Na MWANDISHI WETU – Dar es Salaam
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeteua majina ya Maulid Mtulia na Dk. Godwin Mollel kuwania ubunge katika uchaguzi wa marudio utakaofanyika Februari 17, mwaka huu katika majimbo ya Siha (Kilimanjaro) na Kinondoni (Dar es Salaam) bila kufanyika kwa mchakato wa kura za maoni ndani ya chama hicho.
Mtulia alikuwa mbunge wa Kinondoni kwa tiketi ya CUF na Mollel alikuwa mbunge wa Siha kupitia Chadema, lakini waliamua kuachana na vyama vyao kwa nyakati tofauti mwishoni mwa mwaka jana na kujiunga na CCM kwa kile walichosema kuwa wanaunga mkono mwenendo wa utendaji kazi wa Rais Dk. John Magufuli.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Humphrey Polepole, uamuzi wa kupitisha majina ya wanasiasa hao wageni ndani ya CCM umekuja baada ya tafakuri na tathimini ya kina iliyofanywa na Kamati Kuu (CC) ya chama hicho.
“Baada ya tafakuri na tathimini ya kina, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM na kwa mamlaka iliyokasimiwa kwake na Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), imemteua Dk. …………………………………
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya MTANZANIA.