25.6 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

CCM yailaumu Ukawa

January-MakambaNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimelalamikia kitendo cha Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, kusema watatangaza matokeo yao na kuwaamuru vijana wao waingie barabarani kushangilia.

 

Chama hicho kilisema kauli hizo zinazotolewa na viongozi hao wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ni za hatari kwa amani na usalama wa nchi na ujenzi wa demokrasia na inashangazwa ni kwanini hadi sasa Mbowe na Mbatia hawajaitwa kuhojiwa na mamlaka husika kwa kutoa tishio kwa amani ya nchi.

 

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati akitoa tathimini ya mwenendo wa upigaji kura, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM, January Makamba, alisema viongozi wa upinzani wanasahau kuwa mahakama za kimataifa zimeundwa na zina uwezo wa kuhukumu si tu viongozi walioko madarakani bali hata wale wa upinzani wanaohamasisha fujo na vurugu.

“Tunalaani vikali kauli ya chama kimoja cha siasa kuamua kutangaza kwamba hakitakubali matokeo ya uchaguzi hata kabla matokeo hayo hayajatangazwa, kwa mantiki yao, hakuna haja ya kuwepo kwa NEC.

“Pia Mbowe alisema kama matokeo yao yasipofanana na yale yaliyotokana na kura za wananchi, hawatayakubali.

“CCM inaendelea kusisitiza uamuzi wa Watanzania wanaofanya leo (jana) uheshimiwe na yeyote anayetaka kuvuruga amani ya nchi yetu kwa kisingizio cha kutafuta madaraka asivumiliwe,” alisema January.

Akizungumzia uchaguzi huo uliofanyika jana, alisema katika sehemu kubwa, ulifanyika kwa amani ingawa zimejitokeza kasoro katika maeneo kadhaa. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles