26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

CCM kuwa na vikosi saba kufunga kampeni

makamba NA SHABANI MATUTU, DAR ES SALAAM

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza vikosi saba vitakavyofanya mikutano ya kufunga kampeni zitakazomshirikisha Rais Jakaya Kikwete katika jiji la Mwanza.

Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa CCM anatarajia kuongoza kampeni hizo Mwanza katika mkutano utakaowashirikisha Mgombea urais wa chama hicho, Dk. John Magufuli na Mgombea mwenza, Samia Hassan Suluhu.

Akitaja vikosi hivyo Dar es Salaam jana, Mjumbe wa Kamati ya Kampeni, January Makamba alisema kikosi kingine

kitakuwa Tanga chini ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. Kikosi cha tatu kitakuwa Mbeya

chini ya Rais mstaafu wa awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na cha nne kitakuwa Mtwara kitakachoongozwa na

rais mstaafu awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi.

 

Makamu Mwenyekiti wa CCM, Phillip Mangula ataongoza mapambano katika kikosi cha tano kitakachokuwa Mkoa wa Kigoma wakati Kilimanjaro kitakuwa cha sita chini ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba. Kikosi cha saba kitakuwa Mkoa wa Mara kikiongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba.

January alisema vikosi hivyo saba ni mwanzo wa kazi kwa kuwa wanatarajia kuongeza vikosi kazi zaidi kuanzia kesho

(leo).

“Mikutano hiyo itaanza saa 6.00 mchana na itarushwa yote kwa pamoja kwenye vituo vitano vya runinga na

redio 67.

“Wahudhuriaji wa mikutano hiyo wataunganishwa moja kwa moja kupitia runinga zitakazokuwa katika viwanja

vyote saba itakapofanyika mikutano hiyo kusikiliza hotuba ya Dk. Magufuli atakayoitoa Mwanza,” alisema January.

Alisema ufungaji wa wa aina hiyo wa kampeni ni ya historia na inadhihirisha nguvu ya CCM ya kufanya mikutano

mikubwa ya kampeni kwa siku moja katika maeneo mbalimbali nchini.

“Ukiachilia hilo, tutaweka historia katika tasnia ya utangazaji wa televisheni nchini kwa kutangaza na kuunganisha

matukio saba kwa wakati mmoja,” alisema January.

Kwa Dar es Salaam, alisema wanatarajia kufanya mkutano mkubwa katika uwanja wa Jangwani leo na Jumamosi wagombea ubunge wa mkoa huo watafunga kampeni katika majimbo yao.

AMANI

Akizungumzia kuhusu amani alisema CCM kama chama chenye dhamana ya dola kitahakikisha kinahamasisha

kufanyika uchaguzi wa utulivu kwa wapenzi, mashabiki na wanachama wao.

“Kauli za wenzetu kwamba kura zitaibwa ni za kutojiamini na zenye lengo la kujiandaa kufanya vurugu, na ile ya

kuwataka wanachama wao kukaa vituoni kulinda kura baada ya kupiga kura si watu wanaotaka uchaguzi wa amani,”

alisema January.

January alisema vyama vinatakiwa kutumia utaratibu wa mawakala kwenye vituo husika kulinda kura zao kwa kuwa

ndiyo wenye dhamana ya sheria ya kushuhudia mchakato mzima kuanzia kupiga kura, kuhesabu kura na kutangaza

matokeo.

TATHMINI YA KAMPENI

Akizungumzia kuhusu tathmini ya kampeni January alisema kazi nzuri waliyofanya wagombea wao itawawezesha

kushindwa kwa asilimia zisizopungua 69.

Alisema CCM imeweka utaratibu wa kupokea matokeo kwa kutumia mawakala wake moja kwa moja vituoni na kupitia mtandao wa chama na wanategemea kuwa na matokeo ya uchaguzi nchi nzima ifikapo saa 4.00 usiku ya Oktoba 25, 2015

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles