24 C
Dar es Salaam
Thursday, July 25, 2024

Contact us: [email protected]

Lowassa kuhutubia taifa leo

lowassa-1NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

MGOMBEA urais wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anayeungwa mkono vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa, leo saa tatu usiku anatarajiwa kulihutubia taifa.

Kwa mujibu taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene, hotuba ya Lowassa kupitia vituo mbalimbali vya televisheni, redio na njia nyingine za upashanaji habari ikiwamo mitandao ya kijamii, itajielekeza kuzungumzia mustakabali wa taifa na kutoa shukrani kwa wananchi kumuunga mkono.

“Katika hotuba hiyo kwa taifa, Lowassa atazungumza na Watanzania wote wa ndani na nje ya nchi, na watu
wa mataifa yote kuhusu Tanzania mpya itakayotokana na mabadiliko makubwa ya kimfumo, kiutawala na
utendaji wa Serikali atakayoiunda baada ya Watanzania kumpatia dhamana ya kuwa mkuu wa nchi,
amiri jeshi mkuu na kiongozi mkuu wa Serikali hapo Oktoba 25, mwaka huu,” ilisema taarifa hiyo.

Pia taarifa hiyo ilisema kuwa Lowassa atatumia muda huo kuwashukuru Watanzania wote kwa namna walivyomuunga mkono kwa upendo mkubwa, pamoja na mgombea mwenza wake, Juma Duni Haji na muungano wa Ukawa.

Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa Lowassa atawaelezea Watanzania nia yake ya kuiondoa nchi hapa ilipokwama katika umasikini, ujinga, maradhi na ufisadi unaowatafuna Watanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles