27.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

CARLOS TEVEZ KULIPWA 169,740 KWA KILA DAKIKA

BADI MCHOMOLO NA MITANDAO


carlos-tevezMUNGU akiamua kukunyooshea kidole hakuna mwanadamu ambaye anaweza kutia doa maamuzi yake, maisha yataendelea kwa muda ambao ameupanga yeye.

Mwaka 2016 umemalizika huku Mungu akimnyooshea kidole nyota wa timu ya soka ya Argentina na klabu ya zamani ya Juventus, Carlos Tevez, ambaye alijiunga na klabu ya Shanghai Shenhua inayoshiriki Ligi Kuu nchini China akitokea klabu ya Boca Juniors.

Tevez mwenye umri wa miaka 32 ni mchezaji pekee ambaye kwa sasa anatingisha kwa mshahara katika wanasoka duniani baada ya kujiunga na klabu hiyo ya Boca Juniors kwa mkataba wa miaka miwili.

Mauzo ya mchezaji huyo yamefanyika kwa gaharama ya kitita cha pauni milioni 73, sawa na zaidi ya bilioni 190 ambazo walikubaliana kati ya klabu ya Boca Juniors na matajiri wa nchini China Shanghai Shenhua.

Katika mkataba wa miaka miwili ambao amepewa Tevez utamfanya achukue kitita cha dola milioni 41 kwa mwaka ambapo ni sawa na bilioni 86, wakati huo atakuwa anachukua kitita cha dola 808,000 kwa wiki, sawa na zaidi ya bilioni 1, ikiwa kwa siku ni sawa na dola 115,000 sawa na milioni 244, huku ikiwa sawa na dola 4,800 ambapo ni 10,184,400 kwa saa huku ikiwa kwa dakika akichukua dola 80, sawa na 169,740 kwa dakika.

Hapo ndipo unaweza kusema kwamba mwache Mungu aitwe Mungu, kwa uwezo gani wa mshambuliaji huyo kuweza kusajiliwa kwa kiasi kikubwa kama hicho?    Lakini Mungu alipanga iwe ivyo kwa mchezaji huyo kuja kujiongezea utajiri huku akiwa na umri mkubwa.

Inawezekana mchezaji kusajiliwa kwa kiasi hicho kikubwa cha fedha, lakini klabu mbalimbali zinaangalia umri wa mchezaji mwenyewe, huku wakiwa na lengo la kutaka mchezaji husika kutumia muda mrefu ndani ya klabu akiwa bado ana nguvu za kutosha.

Hadi sasa mchezaji huyo amefanikiwa kucheza jumla ya michezo 503 tangu ameanza kucheza soka la kulipwa mwaka 2001 akiwa na umri wa miaka 17, lakini anakuja kutikisa dunia huku akiwa na umri wa miaka 32, kweli Mungu pekee ambaye anajua kesho yake.

Lakini makubaliano ambayo wameyafikia kati ya klabu ya Boca Juniors na Shanghai Shenhua, ni kwamba endapo mchezaji huyo ataamua kuachana na timu hiyo kabla ya kumalizika kwa mkataba wake wa miaka miwili, basi Boca Junior wanatakiwa kuilipa klabu hiyo kitita cha pauni milioni 41 ambazo ni sawa na zaidi ya bilioni 107.

Hivyo ni wakati wa klabu ya Boca Junior kuonesha heshima kwa mchezaji huyo na kumtakia aendelee kuitumikia klabu hiyo huku akiwa na uhusiano mzuri ili hasiondeke kabla ya mkataba wake kumalizika

Uwezo wa mchezaji huyo ni wa kawaida tofauti na nyota wa sasa ambao wanawika kama vile Lionel Messi wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno, Neymar wa Brazil na klabu ya Barcelona pamoja na wengine wengi kama vile Antoine Griezmann, Luis Suarez na wengine wengi.

Lakini hii imetokea kutokana na nchi ya China kutaka kuliteka soko la soka duniani, huku wenyewe wakidai kuwa hadi kufikia 2020 wanataka kuwa vinara wa soka duniani, hivyo wanasaka saini za nyota wa soka barani Ulaya kwa ajili ya kwenda kuliendeleza soka nchini China.

Mbali na kuwasajili wachezaji wenye majina makubwa barani Ulaya, tayari wameweza kuwateka na makocha wenye majina makubwa kama vile Felipe Scolari ambaye kwa sasa anaifundisha klabu ya Guangzhou Evergrande, Manuel Pellegrini ambaye anaifundisha klabu ya Hebei China Fortune zote zikishiriki Ligi Kuu ya nchini humo.

Hata hivyo mbali na Tevez kusajiliwa kwa kitita kikubwa, lakini nyota mwingine ambaye alikuwa anakipiga katika klabu ya Chelsea, Oscar dos Santos, anadaiwa kusaini mkataba na klabu ya Shanghai SIPG kwa uhamisho wa pauni milioni 60, sawa na bilioni 156, huku akitarajia kulipwa kitita cha pauni 400,000 kwa wiki ikiwa ni sawa na zaidi ya bilioni 1 kwa wiki.

Kwa upande wa Oscar hakuna tatizo kubwa kutokana na mchezaji huyo kuwa na umri mdogo, ambapo mwaka huu Septemba 9, atakuwa anatimiza miaka 26, hivyo bado ana nafasi ya kuendelea kucheza soka kwa muda mrefu. Pia unaweza kusema mchezaji huyo ana bahati kwa kuwa alikuwa hana nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kocha Antonio Conte, lakini matajiri kutoka China wakaamua kukaa mezani na mchezaji huyo nyota wa timu ya taifa ya Brazil na kumfanya awe miongoni mwa wachezaji wanaolipwa fedha nyingi sana kwa wiki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles