27.1 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Cardi B bado yupo matatani

NEW YORK, MAREKANI 

RAPA Cardi B anaendelea kuwa matatani kutokana na tuhuma za kuwashambulia wahudumu wawili wa baa katika moja ya klabu jijini New York, Marekani.

Msanii huyo anadaiwa kuwashambulia wafanyakazi hao wa baa Agosti 2018, hivyo juzi alionekana akiingia kwenye Mahakama ya Queens Supreme kwa ajili ya shitaka hilo.

Inadaiwa kwamba Cardi B baada ya kuwashambulia wahudumu hao siku chache baadaye aliwatishia maisha yao huku mmoja kati yao akimtuhumu kutoka kimapenzi na mume wake Offset.

Mwendesha mashtaka wa kesi hiyo ameweka wazi kuwa, uchunguzi bado unaendelea ili kuweza kukamilisha upelelezi, hivyo baada ya muda Cardi B ataitwa mahakamani kwa ajili ya shitaka hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles