28.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Nicolas Cage amuacha mkewe

CALIFORNIA, MAREKANI 

STAA wa filamu nchini Marekani, Nicolas Cage, ameachana na mke wake, Erika Koike, ikiwa ni miezi mitatu tangu wafunge ndoa.

Machi mwaka huu, wawili hao walifunga ndoa huko Las Vegas nchini Marekani, lakini mapema wiki hii wakathibitisha kuachana kwao.

Cage aliweka wazi juu ya mgogoro wa ndoa yao akidai ulianza siku nne tangu wafunge. Msanii huyo alidai mke wake alikuwa haoneshi ukaribu wa ndoa yao na akaonesha dalili kuwa yupo kwenye uhusiano na mwanaume mwingine. 

“Hapakuwa na uaminifu katika ndoa, siku nne baada ya kuoana, hapakuwa na dalili za upendo ndani yake na nikaja kugundua Erika ana uhusiano mwingine,” alisema Nicolas.

Kabla ya kufunga ndoa na Erika, staa huyo wa filamu mara ya kwanza alifunga ndoa na Patricia Arguette tangu mwaka 1995 hadi 2001, wakati huo mwaka 2002 alifunga ndoa na Lisa Presley, lakini wakaachana 2004 na mwaka 2004 akafunga ndoa na Alice Kim na wakaachana 2016.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,085FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles