CALIFONIA, MAREKANI
MWANAMUZIKI wa hip hop wa Marekani, Cardi B, juzi ameonesha kukonga nyoyo za mashabiki wa muziki wake katika sherehe za Coachella zilizofanyika Ukumbi wa Empire Polo uliopo jijini Califonia, Marekani.
Cardi B ambaye ni mjamzito, alipanda jukwaani kuonesha uwezo wake wa kutoa burudani ikiwa ni siku moja tangu mwanamuziki, Beyonce apande kuungana tena na kundi la Destiny’s Child.
Gumzo kwa mwanamuziki huyo liliongezeka baada ya kuvaa nguo iliyobuniwa na Alejandro sawa na kundi la TLC. Nyota huyo pia alitumbuiza pamoja na kundi la YG, G-Eazy, Chnace The Rapper, Kehlani na 21 Savage.