24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

BUNGE LAZIKA MZIMU WA TRL YAJA NA TRC

Na MAREGESI PAUL

-DODOMA

BUNGE limepitisha sheria ya kulivunja rasmi Shirika la Reli Tanzania (TRL) lililokuwa likimilikiwa kwa mujibu wa sheria na Kampuni ya RITES ya India.

Kwa mujibu was  sheria hiyo mpya, Shirika Hodhi la Mali za Reli (RAHCO) nalo limevunjwa na kuundwa Shirika la Reli Tanzania (TRC).

Bunge jana lilipitisha sheria hiyo ya mwaka 2017  baada ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa  kuwasilisha bungeni Muswada wa Sheria ya Reli ya mwaka 2017.

Akizungumza wakati akiwasilisha muswada huo, Profesa Mbarawa alisema wakati TRL ikimilikiwa kwa ubia na RITES, Serikali ilikuwa ikimiliki asilimia 49 na RITES ilikuwa ikimiliki asilimia 51.

Kwa mujibu wa Profesa Mbarawa, wakati wa ubia huo, TRL ilikuwa haijiendeshi vizuri na uendeshaji huo mbovu ndiyo uliosababisha Serikali kulirudisha Shirika la TRC kwa kuwa lilikuwa likijiendesha kwa faida.

“Kabla TRL haijaja, tulikuwa na TRC ambalo lilikuwa mali ya Serikali lakini kutokana na sababu mbalimbali, Kampuni ya RITES iliingia ubia na Serikali na kuundwa Shirika la TRL.

“Kwa bahati mbaya, TRL halikujiendesha vizuri ndiyo maana tulipoamua kurudisha shirika hilo serikalini tuliamua kutumia jina la TRC ambalo lilikuwa likijiendesha vizuri.

“Kwa hiyo, kwa mujibu wa sheria hii mpya, TRL na RAHCO zimekufa na limeundwa shirika moja la TRC ambalo tunaamini litajiendesha kwa faida kutokana na jinsi tulivyojipanga.

“Ieleweke pia kwamba  mgawanyiko wa   TRL na RAHCO ulikuwa umeshusha utendaji kazi wa shirika ikiwa ni pamoja na kusababisha kushuka utendaji kazi wa Bandari ya Dar es Salaam,” alisema Profesa Mbarawa.

Waziri   alisema madai ya waliokuwa watumishi wa TRL na RAHACO yatazingatiwa kwa kuwa wakati muswada wa sheria unaandaliwa, Serikali iliangalia masuala mbalimbali yakiwamo masilahi ya watumishi wa maeneo hayo.

Wakati huo huo, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, iliishauri Serikali iwe na utaratibu mzuri kwa abiria kupata haki zao   safari za treni zinapoahirishwa kwa sababu mbalimbali.

Katika maoni hayo yaliyosomwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Moshi Kakoso, kamati hiyo ilisema bomoa bomoa inayoendelea nchini kwa waliojenga katika maeneo ya reli, ifanyike kwa umakini wa hali ya juu kwa kuwa baadhi ya wabomolewaji walikuwa wakimiliki maeno yao kwa mujibu wa sheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles