24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 27, 2024

Contact us: [email protected]

BUNGE LAMTIKISA RAIS TRUMP, LAKATAA BAJETI YAKE


WASHINGTON, MAREKANI

SERIKALI ya Marekani chini ya Rais Donald Trump, imeanza kupata mtikisiko hali ambayo itailazimu kufunga huduma zake kwa wananchi kutokana na Bunge la Seneti nchini humo kushindwa kuidhinisha muswada wa bajeti ambao ungeongeza bajeti katika ufadhili wa Serikali Kuu kwa mwezi mmoja.

Taarifa ya Shirika la Utangazaji la Uingereza, imesema bajeti hiyo ilitakiwa kuanza kutekelezwa na Serikali Kuu kuanzia Februari 16, lakini haikupitishwa kutokana na kushindwa kupata kura 60 zinazotakiwa kisheria baada ya mzozo mkali kuhusiana na masuala ya uhamiaji na ulinzi mipakani.

Kushindwa kupitishwa kwa muswada huo kunatokana na mpambano mkali uliopo kati ya vyama viwili vya Republican na Democrat. Awali, Bunge la Kongresi lilipokuwa na wabunge wengi wa chama cha Republican, lilifanya kampeni kubwa ya kukwamisha miswada iliyokuwa ikiwasilishwa na Serikali ya chama cha Democrat, hali kadhalika sasa Democrat wamedhibiti bunge hilo kwa kiasi kikubwa hivyo kuwa kikwazo kwa Serikali ya chama cha Republican.

Kufuatia hatua hiyo, huduma nyingi za Serikali zitakwama, hata hivyo athari kamili itaanza kuonekana kesho, wakati wafanyakazi wa Serikali watarejea kazini.

Mara ya mwisho shughuli za Serikali zilikwama nchini Marekani ni mwaka 2013 na ilidumu kwa muda wa siku 16, wakati ambapo wafanyakazi wengi wa Serikali walishurutishwa kwenda likizo ya lazima.

Ni mara ya kwanza kwa huduma za Serikali kukwama huku chama cha Republican kikidhibiti mabunge yote na Ikulu ya White House.

Kwa upande wao Ikulu ya White House imewalaumu wabunge wa chama cha Democrats kwa kuweka siasa juu ya masuala ya kiusalama, familia za wanajeshi, watoto walio katika mazingira magumu na uwezo wa taifa hilo kuwahudumia raia wa Marekani.

Kiongozi wa wabunge wa chama cha Democrats, Chuch Schumer, alisema Rais Trump alikataa makubaliano yasiyopendelea upande wowote na hakukishinikiza chama chake katika Bunge la Kongresi.

Chama tawala cha Republicans kiliutaja muswada huo kwa jina la ”Schumer Shutdown’ na hawakukosea. Schumer na wabunge wenzake wa chama cha Democrats, wakishirikiana na wabunge wachache wa Republican, walizuia muswada ambao ungesaidia Serikali kuendelea na shughuli zake, hata ijapokuwa kwa muda.

Hata hivyo, kuchukua jukumu na kutoa lawama ni vitu viwili tofauti. Democrats watasema walikuwa wamekubaliana na rais kupitisha muswada usiopendelea upande wowote kuhusu mabadiliko ya sheria ya uhamiaji, kabla ya kukiuka makubaliano hayo wakati wa mkutano Ikulu wiki iliyopita.

Hata hivyo, atakayeshindwa katika mkwamo huu ni chama kitakachoingia katika vita na idadi ndogo ya wabunge ikiwa ni habari mbaya kwa Rais Donald Trump na chama cha Republicans. Habari njema itakuwa kwa pande zote mbili na ngome zao za kisiasa zitafurahishwa kwa kufanya mambo kuwa magumu.

ATHARI ZA KUKWAMA MUSWADA

Suala linalogombaniwa ni lile la chama cha Democrats kutaka zaidi ya wahamiaji wasio na vibali walioingia nchini Marekani kutofukuzwa. Wahamiaji hao walipatiwa vibali vya kuwa nchini humo kwa muda chini ya mradi ulioanzishwa na rais wa zamani, Barack Obama.

Mnamo Septemba mwaka jana, Rais Trump, alitangaza kusitisha mpango huo huku akilipatia bunge la Kongresi hadi Machi mwaka huu kuwa na mpango mbadala.

Wakala wa Serikali Kuu hautakuwa na uwezo wa kufungua ofisi zao licha ya baadhi ya shughuli ndogo ndogo kufanyika. Wafanyakazi kutoka idara za makazi, mazingira, elimu na biashara watatakiwa kubaki nyumbani. Nusu ya wafanyakazi kutoka idara za Hazina, afya, ulinzi na uchukuzi hawatakwenda kazini kesho.

Aidha, idara za hifadhi za taifa na makumbusho nazo zitafungwa hali ambayo inatarajiwa kuibua ghadhabu ya wananchi kama ilivyokuwa mwaka 2013, ambapo wafanyakazi 850,000 walishindwa kwenda kazini. Utoaji wa huduma za hati za kusafiria nao utacheleweshwa.

CHANZO: BBC

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles