22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Bunge lamkingia kifua Naibu Spika  

tulia-acksonNa Khamis Mkotya, Dodoma

BUNGE limemkingia kifua Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson kutokana na namna anavyoandamwa na wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, wakidai anayumbisha Bunge katika kutekeleza majukumu yake.

Kambi hiyo imetangaza kutokuwa na imani na Dk. Tulia, pamoja na kususia vikao vyote vya Bunge atakavyoongoza, kwa kile walichoeleza hawaridhishwi na mwenendo wake, kwani anawaendesha kama wanafunzi.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, alisema msimamo wa wabunge hao wa kutohudhuria vikao vinavyoongozwa na Dk. Tulia hauwezi kuathiri shughuli za Bunge.

Dk. Kashililah alisema uongozi wa Bunge hauoni tatizo la Dk. Tulia na kusema ni kiongozi mahiri anayesimamia kanuni wakati wa kuliongoza Bunge.

Alisema kama wabunge hao wanapinga uamuzi uliotolewa na Dk. Tulia katika jambo fulani, upo utaratibu wa kikanuni unaowapa fursa ya kuulalamikia.

Alisema kama walikuwa hawakubaliani na uamuzi wake wa kuzuia mjadala kuhusu sakata la wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), walipaswa kutumia kanuni ya 5 ibara ndogo ya 4 hadi ya 6 kwa kumwandikia barua Katibu wa Bunge ambaye atawasilisha malalamiko hayo kwa Spika, jambo ambalo hadi sasa hawajafanya.

“Bunge linaongozwa kwa kanuni na huu ndiyo utaratibu, mimi kama Katibu wa Bunge hadi sasa sijapata malalamiko ya mbunge yeyote kutoka kwa mbunge yeyote chini ya kanuni hii. Kwa hiyo wanachokifanya wanajua wenyewe, lakini utaratibu uko wazi,” alisema.

 

NGUVU YA SPIKA

Alisema wabunge wanaweza kuomba mwongozo wa kutaka jambo fulani lijadiliwe au lifanyike, lakini wanapaswa kujua kwamba uamuzi wa Spika ndiyo wa mwisho.

“Kanuni ya 72 (1) inasema Spika atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa utaratibu bora unafuatwa bungeni na uamuzi wa Spika kuhusu jambo lolote la utaratibu utakuwa ni wa mwisho,” alisema.

Alipoulizwa kwanini Naibu Spika hakuruhusu mjadala wa dharura wakati Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari aliomba mwongozo kwa mujibu wa kanuni ya 47 inayotoa fursa hiyo, Dk. Kashililah alisema suala la wanafunzi wa Udom lilikuwa halikidhi vigezo vya udharura.

Alisema vigezo vya hoja ya udharura vimeainishwa katika kanuni ya 48 (4) inayoeleza kuwa jambo lolote litahesabiwa kuwa ni la dharura na lenye masilahi kwa umma iwapo utatuzi wake unategemea hatua zaidi kuliko zile za utekelezaji wa kawaida wa sheria peke yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles