28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

Bunge la DRC lamfuta kazi Spika

KINSHASA, KONGO

Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo(DRC) limepiga kura ya kumuondoa spika wa bunge hilo, Jeanine Mabunda, mshirika wa karibu wa rais mstaafu Joseph Kabila.

Wabunge 484 walihudhuria kikao cha jana jioni kujadiliana iwapo wamuondoe Mabunda katika nafasi ya uspika, huku 281 wakipiga kura ya kumfuta kazi na wengine 200 walipinga uamuzi huo.

Na hatua ya kuondolewa spika huyo inampa Rais Felix Tshisekedi ushindi mkubwa katika mzozo mkali wa kuwania madaraka kati yake na wafuasi wa Kabila. 

Wabunge wa Kongo wamechukua uamuzi huo baada ya kumshutumu Spika Mabunda kwa kuegemea zaidi kwenye mrengo wa kisiasa katika uongozi wake na kutokuwa muwazi linapokuja suala la kusimamia fedha za bunge hilo.

Hata hivyo, spika huyo alikana shutuma zilizotolewa dhidi yake na aliomba radhi kutokana na hali ya kutoelewana iliyojitokeza. Awali, alilisihi bunge kulikataa pendekezo lililowekwa dhidi yake na wafuasi wa Tshisekedi kwa sababu zisizo za kisiasa.

Nguvu kwa washirika wa Tshisekedi

Ushindi huu wa wapinzani wa Kabila ni ishara kubwa ya nguvu ya washirika wa Rais Tshisekedi ambao kwa sasa wanaweza kuwa na wingi wa kutosha ikilinganishwa na baraza la mawaziri ambalo wajumbe wake wengi ni wafuasi wa Kabila. Kura hiyo imepigwa baada ya siku kadhaa za ghasia ndani ya bunge hilo, hatua iliyosababisha polisi kuingilia kati ili kuituliza hali ya mambo.

Rais Felix Tshisekedi(Kushoto) akiwa na Rais mstaafu Joseph Kabila

Wafuasi wa Kabila wa muungano wa kisiasa wa FCC wanamshukutu Tshisekedi kwa kukiuka katiba. Chama hicho kinasema Tshisekedi anapanga njama za kuanzisha utawala wa kidikteta.

”Kila kitu ambacho tumefanya hapa kimekuwa na msingi wa kitapeli. Kwa kweli tulilazimika kulikataa hili ambalo tunaliona hapa na hatukupaswa hata kupiga kura,” alisema Paulin Kashomba ni mfuasi wa Kabila.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles