27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Boti ya mwendo kasi Mwanza-Ukerewe

Na BENJAMIN MASESE

KAMPUNI   Songoro Marine Transport Boatyard  ya Mwanza imesema inatarajia kuwa na chombo cha usafiri kitakachotumia     saa moja kutoka  Mwanza kwenda Ukerewe  badala ya  saa matatu  kama ilivyo sasa.

Kampuni hiyo inayojihusisha kutengeneza   meli, vivuko na  boti

Akizungumza na waandishi  wa habari jana, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Major Songoro alisema wameamua kuwa na chombo chao cha usafiri  kitakachotumia muda mfupi kwenda Ukerewe na sehemu nyingine.

Songoro alisema boti inayojulikana kwa jina la RAFIKI .1 ina uwezo wa kubeba abiria 200 na imegawanyika sehemu mbili za abiria wa kawaida na daraja la juu (VIP) ambako kila abiria anakuwa na kiti cha kisasa.

“Kazi yetu ni ujenzi wa meli, vivuko, vivuko na ukarabati wa vyombo vya majini.

“Shughuli hii tunaifanya kwa kiwango kikubwa   na ndiyo maana Serikali tunashirikiana kuhakikisha  tunaimarisha ubora na usalama wa raia katika vyombo  vya majini.

“Hatujawahi kumiliki meli kubwa ama boti licha ya sisi kuvitengeneza na tumeamua kuanza na boti hii ya kisasa.

“Kama mlivyoiona  ilivyojengwa ndani na kuwa na viti vya abiria vizuri tena vya kukaa na kuzunguka hasa VIP, kwa wale waliobahatika kusafiriki kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar kwa kutumia boti za Kilimanjaro wanajua raha yake.

“Kwa uwezo wa boti hii, mfano kutoka Mwanza kwenda Ukerewe itatumia saa moja tu, tunataka kuleta maajabu ya kuwaondolea  abiria kukaa muda mrefu majini.

“Kwa ratiba tuliyonayo kama tutakamilisha mambo yetu na Serikali nadhani  Desemba mwaka huu kitakuwa kinafanya safari na tutaweka wazi wapi kitakuwa kinakwenda na gharama zake,”alisema Songoro.

 

Hata hivyo alivyoulizwa sababu za kutoshinda zabuni za ujenzi wa meli kubwa zinazotangazwa na Serikali, Songoro alisema  uwezo wanao wa kutengeneza chochote kile ambacho kinatakiwa  hivyo aliiomba Serikali kuwaamini.

Wakati huo huo, Kivuko cha MV Chato kilichokuwa kikifanyiwa ukarabati katika yadi hiyo kwa gharama ya Sh milioni 61 kimekamilika na kuondoka kuendelea na safari zake huku MV Sengerema inayokarabatiwa kwa Sh milioni 589 ikitarajiwa kufanyiwa maboresho kwa miezi mitatu ili kurejea Kigongo-Busisi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles