25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Benki yatoa matreka ya bilioni 2/-  kwa wakulima wa pamba

Na Mwandishi Wetu

BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania(TADB) imetoa matrekta 50 yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 2.7  kwa Vyama vya Ushirika 50 vya Msingi vya Masoko (AMCOS) vinavyolima  pamba katika mikoa ya Kanda ya Ziwa  kuongeza tija na uzalishajji wa zao hilo.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Japhet Justine amesema TADB inalenga  kuwawezesha wakulima wa   pamba hapa nchini  waweze kuongeza tija na uzalishaji kama inavyobainishwa katika Mpango wa  Mandeleo ya  Kilimo Awamu ya Pili(ASDP-11).

“Matreka ni moja ya nyenzo itakayowawezesha wakulima kuongeza uzalishaji kwa kulima maeneo makubwa zaidi kwa kufuata kanuni bora za kilimo cha pamba tofauti na kutumia  jembe la mkono,”  alisema Justine

Alisema matrekta ni sehemu ya utekelezaji wa  ASDP -11 katika kuhakikisha nyenzo bora za kilimo zinawafikia wakulima na kuchagiza uzalishaji zaidi wa malighafi zitakakazotumika kwenye  viwanda  na kufanikisha azma ya serikali ya kujenga uchumi wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025.

“TADB ndiyo benki yenye dhamana kubwa kwa mkulima hivyo tutaendelea kuboresha mazingira katika sekta ya kilimo kwa kutoa mikopo kwa wakati, nyenzo za kilimo lengo likiwa kumtoa mkulima katika kutumia jembe la mkono,” alisema Justine

Alisema maeneo mengi   nchini bado wakulima wanatumia jembe la mkono linaloendelea kudumaza sekta kwa kufanya kilimo cha mazoea hivyo benki benki imejipanga kuwa mkombozi wa mkulima na kufanya kilimo biashara kupitia huduma mbalimbali tutakazozitoa.

“Tumeanza na wakulima wa pamba kwa kuwapatia matreka kupitia vyama vyao na tutaendelea katika maeneo mengine  kuhakikisha mazao yote ya kipaumblele yanatengenezewa mazingira bora ili uzalishaji  wake uongezeke,” alisema Justine

Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba, Marco Mtunga alisema   kupitia mkopo wa viuadudu uliotolewa msimu uliopita na TADB, ambako uliwanufaisha zaidi ya wakulima 600,000  wa   pamba umewezesha kuongeza uzalishaji kufikia tani 221,600 ikiwa ni ongezeko la asilimia 67 ikilinganishwa na tani 133,000 zilizozalishwa msimu wa 2017/18.

“TADB  mkombozi wetu wa kweli  kwani amefanikisha  upatikanaji wa pembejeo kwa wakati na kuongeza uzalishaji wa zao la pamba ,” alisema Mtunga

Mmoja wa wakulima walionufaika na matrekta hayo, Amina Makoma aliishukuru serikali kupitia benki ya maendeleo ya kilimo kwa kuweza kuwakopesha matrekta hayo hali itakayoongeza uzalishaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles