26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Bongo Fleva wafunika Serebuka Festival 2016

Ali Kiba
Ali Kiba

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

NYOTA wa Bongo Fleva, Ali Kiba, Judithi Wambura ‘Jay Dee’ na Boniventure Kabogo ‘Stamina’, wamenogesha tamasha la Serebuka Festival kwa shoo kali ya maadhimisho ya miaka miwili ya chaneli ya Star Time Swahili inayoruka kupitia king’amuzi cha StarTime.

Mbali na Ali Kiba na Stamina, wasanii wengine walionogesha tamasha hilo ni Yamoto Band, Dogo Niga, Sara Kaisi ‘Shaa’, Jokate Mwegelo, Snura Mushi, Juma Nature, HK, Jacob Steven ‘JB’ na Ray Kigosi.

Tamasha hilo lililofanyika jana kwenye viwanja vya Posta Kijitonyama jijini hapa, liliandaliwa na kampuni ya matangazo ya Blueline kwa kushirikiana na Huawei Tanzania.

Msemaji wa Blueline ambao ndio waandaaji wakuu wa tamasha hilo, Leonard Mtabuzi, aliwashukuru mashabiki waliojitokeza na kuahidi mambo mazuri zaidi yatakayoandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya wateja wao.

“Huu ni mwanzo tu kuna mambo mengi mazuri yanakuja kutoka Blueline, tumeona wasanii wengi juu ya jukwaa moja na walichokifanya mashabiki wamekipenda ndiyo maana wakati wote walikuwa wakiwashangilia, napenda kuwashukuru na kuwaahidi mambo mazuri zaidi kwa ajili yao yanakuja,” alimaliza Mtabuzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles