29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Bodi ya Pamba yaanza kusambaza mbegu kwa wakulima Bariadi

Derick Milton, Bariadi



Bodi ya Pamba nchini imeanza kusambaza mbegu ya zao hilo kwa wakulima wilayani hapa, ambapo zaidi ya magari makubwa 30 yenye tani zaidi ya 350 za mbegu hizo yamewasili tayari kwa shughuli hiyo.

Hatua hiyo inatokana na agizo la Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga, alilolitoa siku mbili zilizopita kwa bodi hiyo kuhakikisha inaongeza mbegu za pamba baada ya kuwapo kwa malalamiko mengi ya wakulima kukosa mbegu hizo.

Ijumaa ya Wiki hii, mkuu huyo wa Wilaya alitoa siku saba kwa bodi hiyo kuhakikisha wakulima wote ndani ya wilaya hiyo wanapata mbegu za kutosha kwa ajili ya kilimo cha zao hilo ambacho msimu wake wa kulima umeanza.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Bariadi leo Jumapili Novemba 18, akiwa na Magari zaidi ya 30 yenye mbegu hizo, Mkurugenzi wa bodi hiyo, Marco Mtunga, amesema kuwa zaidi ya tani 350 zimeingizwa jana na leo.

“Haya ni baadhi ya magari zaidi ya 30 ambayo toka jana yameanza kuingia Bariadi na mengine tayari yamefika vijijini kugawa mbegu.

“Magari haya yamebeba zaidi ya tani 200 na tayari tumesambaza tani 120, tuwahakikishie wananchi hata kama hizi ambazo tumeleta leo zikiisha tutaongeza nyingine maana bado mbegu tunazo nyingi, lakini tuna imani hizi tulizoleta zitatosheleza mahitaji,” amesema Mtunga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles