26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Bobi Wine aanza kampeni za kumng’oa Museveni

KAMPALA, UGANDA

MBUNGE wa Kyadondo Mashariki, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine juzi alianza kile kinachoonekana kampeni za kumng’oa Rais Yoweri Museveni.

Akiwa katika Wilaya ya Ntungamo aliwahamasisha vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura iwapo wanataka kuona ndoto zao za uwapo wa mabadiliko ya uongozi wa nchi katika Uchaguzi Mkuu wa 2021 inatimia.

Mwanamuziki huyo aliyegeukia siasa ana wafuasi wengi vijana, ambao pia ndio kundi kubwa zaidi la wapiga kura nchini humo.

Bobi Wine alisema hayo wakati alipozungumza na vijana waliojitokeza kumwona na kutaka kumsikia katika Mji wa Rubaare wilayani humo muda mfupi baada ya kuhudhuria misa katika Kanisa la All Saints.

Bobi Wine alitumia mapumziko ya mwishoni mwa wiki katika mji huo, ambapo alihudhuria shughuli ya kimila inayomhusu shemeji yake.

Akiwa ameandamana na baba mkwe wake Dk. Joseph Kagaju, mkewe Babra Itungo na wanafamilia wengine aliingia kanisani saa 4:40 asubuhi, ambako wakati akitoa hotuba yake fupi alikwepa kuzungumzia siasa.

“Nina bahati sana kuwa kanisani hapa, nawapenda sana watu wa Rubaare, sitazungumzia siasa kwa sababu nipo na watu wasioipenda,” alisema Kyagulanyi.

Muda mfupi baada ya hotuba yake, Bobi Wine aliondoka na msafara wake ambao ulisimama katika Kituo cha Mafuta cha Caltex mjini Rubaare.

Mara ghafla gari lake likazungukwa na umati wa vijana waliotaka kupiga naye picha huku wakimshinikiza azungumze siasa na sana sana mabadiliko ya uongozi.

Alijaribu kuwakwepa hilo mara kadhaa akiondoka kutoka garini kwenda maliwato, gereji na kisha kurudi garini mwake.

Akiwa garini akaamua kutokezea juu ya gari na kuwahutubia, akiwataka wafanye kweli iwapo wanataka mabadiliko hayo kwa kuanzia kujiandikisha kwa wingi katika daftari la kura, akionya bila hivyo itakuwa kazi bure.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles