23.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Blac aichokoza familia ya Kardashian

rob-kardashian-blac-chyna-inline-5755b8b7-5187-4992-abe7-713d8adc6858NEW YORK, MAREKANI

MWANAMITINDO maarufu nchini Marekani, Blac Chyna, amejitosa kuichokoza familia ya Kim Kardashian baada ya kutoka kimapenzi na kaka wa Kylie Jenner, Kim na Khole, ambaye anajulikana kwa jina la Rob Kardashian.

Mrembo huyo awali alikuwa anatoka na rapa Tyga na kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume. Tyga kwa sasa anatoka na mdogo wao Kim Kardashian, Kylie Jenner, wakati huo Blac yeye ameamua kutoka na kaka wa Kylie, Rob Kardashian.

Kitendo hicho ni wazi kwamba ataleta mgogoro na Kylie, ambaye kwa sasa anaishi na Tyga, mume wa zamani wa Blac.

Hata hivyo, Blac amedai hana wasiwasi na jambo lolote kwa kuwa wao wamependana na wanaweza wakaoana baadaye.

“Najua yataongelewa mengi, lakini sipo kwa ajili ya kugombana na mtu na ninaamini wenyewe tumependana na tunaweza kuoana,” aliandika Blac kwenye mtandao wa Instagram.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles