23.4 C
Dar es Salaam
Friday, June 21, 2024

Contact us: [email protected]

Chris Brown ashinda kesi yake

chrisbrown-624-1364310200LAS VEGAS, MAREKANI

NYOTA wa muziki nchini Marekani, Chris Brown, amefanikiwa kushinda kesi yake ya madai kwamba alimpiga mwanamke na kumpokonya simu yake walipokutana kwenye Kasino mwanzoni mwa mwezi huu.

Mkuu wa sheria katika Jimbo la Las Vegas, Steve Wolfson, amesema kuwa hakuna ushahidi wa kutosha wa kumfungulia msanii huyo mashtaka ya utovu wa nidhamu kwa kumshambulia mwanamke huyo na kumuibia simu.

Hata hivyo, msemaji wa msanii huyo alikanusha madai ya mwanamke huyo akisema kuwa si ya kweli na yalikuwa na lengo la kumharibia msanii huyo.

Mwaka 2009, Brown alitakiwa na Mahakama kukaa miaka mitano bila kufanya kosa lolote, baada ya kupatikana na hatia ya kumpiga nyota wa muziki wa pop, Rihanna, ambaye alikuwa mpenzi wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles