27.9 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

Biteko atoa onyo la mwisho migogoro kweye migodi

Na Derick Milton, Simiyu

Waziri wa Madini, Dotto Biteko ametoa onyo la mwisho kwa baadhi ya wafanyabiashara wa madini ambao wamekuwa chanzo cha migogoro kwenye migodi midogo nchini.

Biteko ametoa kauli hiyo leo Jumamosi, Desemba 19, mbele ya wachimbaji wadogo wa mgodi wa Rubaga, ulioko mpakani mwa Wilaya ya Busega na Bariadi mkoani Simiyu.

Amesema migogoro kwenye migodi midogo imezidi na imekuwa kero ambapo ameeleza baadhi ya wafanyabiashara ndiyo wamekuwa chanzo cha migogoro hiyo.

“Tunayo majina ya baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa chanzo cha migogoro kwenye migodi hii midogo imezidi, imekuwa kero, kila siku migogoro, tumechoka.

“Tunajua wanaanzisha hii migogoro ili waweze kutorosha madini, nawaambia siku zao zimefika, wamefanya uko, sasa wameanzisha huku Simiyu, serikali hatuwezi kuwavumilia,” amesema Biteko.

Hata hivyo, Biteko amesema kuwa bado kwenye migodi midogo midogo, utoroshaji wa madini umekuwa mkubwa, hivyo amewataka viongozi wa mkoa na Wilaya kusaidia katika kudhibiti wizi huo.

Amesema kuwa wizara yake imeanza kuchunguza watu wote ambao wanafanya vitendo hivyo vya kutorosha madini, kwani majina yao wanayo na watachukuliwa hatua kali mmoja mmoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles