27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

BILIONI 5 KUBORESHA AFYA YA MAMA NA MTOTO MARA

Na Mwandishi Wetu -Mara

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeupatia Mkoa wa Sh bilion 5.9 kwa ajili ya kuboresha huduma za afya kwa wananchi katika mkoa huo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile amesema hayo leo Ijumaa Julai 20, akiwa katika ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara.

Aidha, akiwa ziarani mkonai humo Dk. Ndugulile ameagiza Kamati ya Ulinzi ya Wilaya ya Tarime ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya, Vincent Naano kusimamia vizuri manunuzi ya dawa, huku akimtaka Mganga Mkuu wa Mkoa Dk. Mwanisi kuhakikisha  dawa zote zinunuliwe kutoka Bohari ya Dawa (MSD).

“Utaratibu wa kuagiza dawa kwa mawakala sitaki kuusikia, MSD tuna dawa karibia zote za msingi, utaratibu wa mawakala tuliuweka kama mbadala endapo MSD watakosa aina fulani ya dawa,” amesema Dk. Ndugulile.

Aidha, kuhusu mimba za utotoni, Dk. Ndugulile bado ni tatizo kubwa ambapo Mkoa wa Mara ni wa tano kitaifa kwa kuwa na asilimia 37.

“Serikali imeandaa mpango wa kazi wa kitaifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa mwaka 2017/18-2021/22 na moja kati ya msisitizo katika mpango huu ni kutokomeza ukatili wa kijinsia shuleni,” amesema Dk. Ndugulile.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles