26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Bilioni 5.2/- kujenga barabara Nzega

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Selemani Jafo
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Selemani Jafo

NA GABRIEL MUSHI,

SERIKALI imesema inatarajia kutumia   Sh bilioni 5.2 katika ujenzi wa barabara ya kilomita 10 mjini Nzega  katika bajeti ya halmashauri ya mwaka 2017/18.

Kauli hiyo ilitolewa bungeni  Dodoma na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Selemani Jafo, wakati akijibu swali la Mbunge wa Nzega Mjini, Husein Bashe (CCM).

Mbunge huyo aliuliza  ni lini serikali itaanza   ujenzi wa barabara hiyo kama ambavyo Rais John Magufuli alivyoahidi wakati wa kampeni.

Jafo alisema hatua za awali za utekelezaji wa ahadi hiyo ya Rais ya kujenga kilomita 10 za barabara kwa kiwango cha lami zimeshaanza.

Alisema  kazi iliyofanyika ni upembuzi yakinifu, usanifu wa kina, kuandaa michoro na makisio ya kazi za ujenzi wa kilomita zote 10.

“Mtandao huo wa barabara utajengwa katika kata za Nzega Mjini Mashariki sawa na kilomita tano kata ya Nzega Mjini Magharibi kilomita tano zilizobaki.

“Gharama za utekelezaji mradi huo ni Sh bilioni 5.2 zitahusisha ujenzi wa mitaro ya barabara na makalvati ikiwamo mitaro mikubwa katika eneo la Samora, ujenzi matabaka ya barabara ya changarawe na ujenzi wa matabaka mawili ya lami nyepesi,” alisema.

Licha ya Bashe kuuliza swali la nyongeza kuwa serikali haioni haja ya kujenga barabara hiyo kwa fedha za Tanroads kuliko kutegemea mapato ya halmashauri ambayo ni kidogo sawa na Sh bilioni 5.7, Naibu waziri   alisema suala hilo litatekelezwa kama ilivyopangwa kwa kuwa ilikuwa na uamuzi wa serikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles