30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mkurugenzi awatumbua walimu wawili

Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako
Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako

Na IBRAHIM YASSIN, ILEJE

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje, mkoani Songwe, Haji Mnasa, amewavua madaraka walimu wakuu wawili wa shule mbili tofauti kutokana na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka, ubadhirifu wa fedha za shule na utoro kazini.

Akizungumza na waandishi wa habari wiki iliyopita, Mnasa alisema amewachukulia hatua walimu hao baada ya kujiridhisha juu ya tuhuma zao.

Aliwataja walimu hao kuwa ni Henry Musomba, aliyekuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Ibaba na Emecka Minga, aliyekuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Ngulungulu.

“Walimu hao walikuwa wakifanya kazi kwa mazoea, kwani walikuwa wazembe na inasemekana walikuwa wakitoa lugha chafu kwa walimu wenzao na kwa wazazi wa wanafunzi pindi wanapokwenda shuleni hapo kuzungumzia masuala mbalimbali.

“Baada ya kupata tuhuma hizo, tuliunda timu ya uchunguzi ambayo baada ya kuchunguza jambo hilo kwa kina, ilikuja na majibu ya kuwepo kwa hali hiyo.

“Timu hiyo ya uchunguzi iliandika ripoti na kuikabidhi kwa mwenyekiti wa halmashauri na nakala ilikabidhiwa kwa mkuu wa wilaya kwa ajili ya uamuzi.

“Baada ya hapo, mwenyekiti wa halmashauri aliwaeleza madiwani wa halmashauri hiyo kupitia kikao cha baraza kilichokaa wiki iliyopita ambapo madiwani hao walibariki uamuzi wa kuwachukulia hatua walimu hao,” alisema Mnasa.

Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Ubatizo Songa, alisema  aliwahi kupata taarifa mbaya za watumishi hao, lakini alishindwa kuwachukulia hatua kwa kuwa si mwajiri wao.

“Nilichokifanya baada ya kupata taarifa hizo ni kutoa taarifa kwa mkurugenzi mtendaji kwa sababu ndiye mwajiri wao ambaye leo ametangaza hatua alizochukua.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya hiyo, Joseph Mkude, alisema uamuzi wa madiwani kupitia mkurugenzi mtendaji kuwashusha vyeo walimu hao ni sahihi kwani utajenga nidhamu ya utumishi serikalini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles