25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Bibi wa Obama afariki Kenya, Uhuru aongoza wakenya kutoa salamu

Nairobi,Kenya

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta pamoja na Viongozi wengine wameendelea kutoa salam za rambirambi kufuatiwa kifo cha Bibi wa Rais wa zamani wa Marekani, Barrack Obama.

Kifo hicho cha Bibi Sara Obama kimetokea leo Machi 29, 2021 katika Hospitali moja Magharibi mwa Kenya baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Pia Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga, amemzungumzia Sara Obama kwa kuwa nguzo ya familia baada ya kifo cha mume wake na kutumia nafasi ya mjukuu wake Obama kwa kuimarisha masomo kwa watoto wa kike na kukabiliana na maovu katika jamii.

Hata hivyo Dada wa Rais Obama, Auma Obama kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii Twitter ameandika kuwa amepatwa na simanzi kufuatia kifo cha Bibi yake na alibarikiwa kuwa na ukaribu naye kwa muda mrefu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles