29.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

Uganda yatangaza kutengeneza Chanjo ya Covid 19

-Uganda

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ametangaza mchakato wa kutengeneza chanjo ya Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu (Covid 19) ambayo inatarajiwa kuanza Kufanyiwa Majaribio mwezi Juni mwaka huu.

Majaribio hayo yanatarajiwa kufanyika kwa Panya na baadae kufanyiwa majaribio nyani mwezi Agosti mwaka huu na kisha kusubilia kuthibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Rais Museveni ameyasema hayo wakati akichomwa Sindano ya Chanjo ya Covid 19 pamoja na mke wake  Janet Museveni katika Ikulu ya Rais Nakasero Mjini Kampala.

Pia ametoa wito kwa Wananchi wa Uganda kujitokeza kupata chanjo kwa kusema haina Madhara yeyote kiafya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles