24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Biashara kuuziana umeme Afrika Mashariki kizungumkuti

bwawa-la-umeme-mto-nile-ethiopiaNa Mwandishi Wetu

Mpango wa kuuziana umeme Afrika Mashariki unaonekana kukwana kutokana na sababu mbalimbali na kusababisha miradi ya viwanda katika nchi hizo kushindwa kuanza kwa kukosa nishati ya umeme.

Sababu  za kuleta hali hiyo ni nyingi lakini kubwa  ni ile ya  kukwama miradi ya kuzalisha umeme kuchelewa kukamilika na zingine ni ukame, kuchelewa kusaini mikataba na kukosa fedha za kuendeleza miradi husika na  vilevile kukosa hisani za wafadhili.

Kutokana na ukata Rwanda, Kenya na Uganda itabidi wasubiri sana kabla hawajaanza kufanya biashara rasmi ya kuuziana umeme kwa kukosa umeme wenyewe kwani miundombinu yake haijakamilika na haijulikani lini itakuwa tayari.

Kule Rwanda makandarasi bado hawajakamilisha ujenzi wa vituo vya kupozea umeme na ile ya nyaya za umeme mkubwa (higher voltage lines) kutokamilika na kufanya tarehe ya kuanza mwaka jana kusogezwa mbele mwaka huu Aprili na sasa wahusika hawasemi lini utakamilika kwani bado.

Mradi huo wa umeme ni sehemu ya Miradi ya utangamano (Coalition of the Willing) kwa kile kinachoitwa Miradi ya Miundo mbinu ya Korida ya Kaskazini ya Afrika Mashariki inayohusu nchi hizo tatu, Sudan na Ethiopia.

Mkuu wa Uganda Electricity Transmission Company Ltd Erias Kiyemba alisikika na vyombo vya habari akisema kuwa makandarasi wamekuwa kikwazo kikubwa cha miradi ya nishati kwa nchi zote tatu na hivyo kukwamisha shughuli za biashara ya kuuziana  umeme.

“Lazima miundombinu ikamilike kwanza kwani nishati haiwezi ikaruka,” alisema Elias Kiyemba.

Kwa kifupi miradi bado ni vipande vipande kwani  Rwanda imemaliza kujenga nyaya za umeme  mkubwa wa 220 kv ya kuunganisha ummeme kutoka Uganda ya Magharibi wakati Kagitumba –Mirama hadi Shango ulimalizika mwaka jana mwezi Oktoba na mipango iliyopo sasa ni kukamilisha shughuli hiyo mwishoni mwa mwaka huu.

Kwa ujumla miradi hiyo imekamilika kwa asilimia 90 baada ya kandarasi kuamriwa aongeze juhudi ya kazi na kukamilisha mapema iwezekanavyo.

Mkandarasi wa Uhandisi toka Spain Isolux Ingenieria,  kampuni iliyopewa  kazi kujenga umeme na hizo nyaya kuu na vituo vya kupoza haikuwa  wazi kuelezea kwa nini mradi unasuasua.

Lakini minong’ono kwenye sebule za madaraka inasema kampuni hiyo imezidiwa kazi kwani inakazi pia huko DR Congo, Uganda na Tanzania .

Kutokana na ripoti ya Benki ya Dunia ni kwamba Rwanda ndio inapata matatizo mengi ya kukatika umeme zaid ya mara 14 kwa mwezi na hivyo miradi hiyo ni muhimu kwa uchumi wake na ushindani wa kibiashara katika eneo hili. Matatizo huwa makubwa zaidi katika kipindi cha Juni hadi Agosti ambapo ukame huwa mkubwa na mahitaji ya umeme kuwa makubwa zaidi.

Hali katika nchi nyingine Afrika Mashariki sio nzuri sana ambapo Burundi na Tanzania umeme hukatika mara 12 wakati Uganda mara 11 na Kenya mara 7 kwa mwezi. Lakini ripoti hiyo haianishi lini ilifanyika kwani kuna uboreshaji mkubwa wa upatikanaji umeme Tanzania.

Utegemezi wa umeme wa maji Tanzania umepungua kutoka asilimia 70 hadi 20 wakati Rwanda inategemea mafuta mazito kwa asilimia arobaini na gesi asilia kutoka Ziwa Kivu na mitambo midogo ya sola huchangia kidogo na kufanya umeme wa maji uwe na mchango wa asilimia 50.

Kuagiza umeme kutoka nje ni suluhisho muafaka kwa Rwanda na hivyo kadiri mpango wa mauzo unavochelewa unakera kwa kila mhusika. Kimipango Rwanda iliazimia kuagiza umeme wa MW15 kutoka Uganda, MW 30 toka Kenya na MW 400 toka Uhabeshi ili kukidhi mahitaji yake ya sasa na baadaye.

Uhabeshi (Ethiopia) inaonesha kwa muda mrefu itakuwa na ziada ya umeme na kutokana na hilo Tanzania imetiliana saini nayo  ya kuuziwa umeme wa MW 400 wakati ikiendelea kujenga mitambo ya kuchakata umeme wa kutumia  gesi asilia     sehemu mbalimbali za nchi.

Mwaka jana pekee Uhabeshi ilipata jumla ya dola milioni 123 kutokana na mauzo ya umeme kwa nchi mbalimbali kutokana na  umeme kutoka maji ya Mto Nile katika miezi nane ya 2015/2016 na kuonekan kuwa ni biashara nzuri kwani inalipa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles