Na BEATRICE KAIZA, Mtanzania Digital
KAMPUNI ya Kimataifa michezo ya kubashiri ya BetWay, imezinduliwa Tanzania, huku ikijipanga kuunga mkono jitihada za Serikali za kuendeleza soka kuanzia ngazi za chini na kuwapa burudani mashabiki mchezo huo.
Hayo yamesemwa na Meneja Uendeshaji, Jimmy Masaoe alipozungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Amesema Betway ni kampuni ya kubashiri iliyosajiliwa Tanzania, huku ikiwa ni mdhamini wa klabu ya West Ham United ya England.
“Ni wakati mzuri katika sekta ya michezo ya kubashiri na tunaamini kwa uzinduzi wa bidhaa hii yenye ubora wa kimataifa kwenye soko, tunauwezo wa kuleta msisimko kwa wanaobashiri na mashabiki, wakati bado tunarudisha kwa jamii kupitia miradi mbali mbali ya michezo.”
“Betway tumejipanga kuwekeza zaidi Tanzania kwa lengo la kukuza na kuendeleza mchezo wa soka na leo rasmi tumefanya uzinduzi, tunahakikisha tunazifikia hadi timu za madaraja ya chini,” amesema Masaoe.
Kwa upande wa Meneja Masoko wa kampuni hiyo nchini Tanzania, Calvin Mhina, amesema kuwa kuisapoti michezo katika jamanii ni kitu cha muhimu.