BENKI YA WANAWAKE NCHINI KUFUMULIWA

0
778

Rais John Magufuli, amesema watapitia upya na kuchambua uongozi wa Benki ya Wanawake nchini (TWB), ili benki hiyo iweze kufanya kazi kiushindani.

Rais Magufuli amesema hayo leo Desemba 8, mjini Dodoma wakati akizindua mkutano wa tisa wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na kuongeza kuwa benki hiyo imekuwa ikimkandamiza mwanamke hasa katika mikopo kwa kulipia riba kubwa na wakati huo huo wanufaika wengi wa mikopo hiyo ni wanaume.

“Tutapitia upya na kuichambua Benki ya Wanawake, hatuwezi kuwa na benki inayowaumiza wanawake tutaiangalia ili iende vizuri kiushindani, hatuwezi kuwa na benki ambayo inafanya ufisadi tu isiwe chombo cha kuleta hasara kwa fedha ambazo zingeweza kwenda kwenye kilimo lakini wanaokopa pale ni wanaume,” amesema Rais Magufuli.

Pamoja na mambo mengine, Rais Magufuli ameutaka uongozi mpya atakaouchagua kumsaidia kufanya mabadiliko katika benki hiyo ili ifanye kazi kwa ufanisi na ushindani.

“Kumekuwa na kawaida kuwa benki hii kila anapokuwa mwanamke haifanyi vizuri badala yake imekuwa ya kuwanyonya wanawake, nimesema haya na ni matumaini yangu mmenielewa,” amesema.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here