23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Benki ya Exim yatoa Sh milioni 10 kusaidia ujenzi vyoo vya shule Zanzibar

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Benki ya Exim imetoa kiasi cha Sh milioni 10 kwa taasisi ya Asma Mwinyi Foundation (AMF) kwa ajili ya kuwezesha ununuzi wa vifaa vya ujenzi na ukarabati wa vyoo vya Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Kandwi iliyoko Unguja, Zanzibar.

Hatua hiyo ni sehemu ya dhamira endelevu ya benki hiyo katika kusaidia sekta za elimu na afya nchini.

Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim, Stanley Kafu (wa nne kushoto) akiwasilisha mfano wa hundi yenye thamani ya Sh mil 10/-  kwa Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Asma Mwinyi Foundation (AMF), Asma Mwinyi (wa tatu kulia) kwa ajili ya kuwezesha ununuzi wa vifaa vya ujenzi na ukarabati wa vyoo vya Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Kandwi iliyoko Unguja, Zanzibar. Wanaoshuhudia ni pamoja na Meneja Mwandamizi wa benki ya Exim Zanzibar, Mwinyimkuu Ngalima (wa tatu kushoto), maofisa wa benki hiyo pamoja na wawakilishi wa shule hiyo.

Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim, Stanley Kafu, aliwasilisha msaada huo kwa, Asma Mwinyi ambaye ni Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi AMF katika hafla ya makabidhiano ambayo ilifanyika katika viwanja vya shule hiyo mapema hii leo Zanzibar.

“Tumejitolea kuhudumia watu, biashara na jamii kwa ujumla. Benki ya Exim na AMF kwa pamoja tuna dhamira inayofanana ya kusaidia juhudi za kielimu na ustawi wa wanafunzi wetu na shule kote nchini. Wanafunzi hutumia muda mwingi zaidi katika siku wakiwa shuleni hivyo ni muhimu zaidi tukiweka jitihada katika kuboresha mazingira ya vyoo vyao,” alisema.

“Tunafurahi kuwa sehemu ya mkakati huu muhimu unaolenga kuinua mazingira ya elimu Zanzibar. Tunaona kwamba taasisi ya AMF kuwa mshirika sahihi katika kufanikisha dhamira hiyo. Benki ya Exim tumekuwa wadau wakubwa katika kusaidia sekta ya elimu katika jamii yetu, na tunatarajia kupanua juhudi hizo hapa Zanzibar,” aliongeza.

Ikiwa ni taasisi isiyojiendesha kibiashara yenye makao yake nchini, AMF imejikita zaidi katika kukuza programu ambazo zinaboresha maendeleo ya jamii katika mazingira ya vijijini na mijini, kushughulika haswa na wasichana na wanawake wenye mahitaji ya elimu, afya, na mahitaji mengine ya msingi katika jamii zao.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya AMF, Asma Mwinyi aliishukuru benki ya Exim huku akibainisha kuwa msaada huo utagusa maisha ya wanafunzi wengi kwa miaka mingi ijayo.

“Wadau wetu muhimu na washirika kama Benki ya Exim ndio nguzo muhimu kwa mafanikio yetu. Tunashukuru kwa msaada huu ambao utasaidia katika kukarabati vyoo vya Shule ya awali, Msingi na Sekondari ya Kandwi,” alibainisha.

Kulingana na taarifa ya wasemaji wa shule hizo, Kheir Juma Pandu na Juma Haji Ame walieleza kuwa, kukamilika kwa ujenzi na ukarabati wa vyoo hivyo kutasaidia kuhudumia wanafunzi zaidi 700 waliopo katika shule hiyo.

“Tunatumahi kuwa ukarabati huu utasaidia watoto kuzingatia kwa zaidia masomo yao,” walieleza.

Zaidi alitoa wito kwa taasisi zingine za kifedha na wadau wanaopenda kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha mazingira ya kujifunzia katika shule za umma nchini kujitokeza kwa wingi katika jitihada hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles