25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

BENJAMIN NETANYAHU AHOJIWA NA POLISI KWA RUSHWA

YERUSALEM, ISRAEL


benjamin-netanyahu12WAZIRI Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amehojiwa na polisi wanaochunguza madai kuwa alipokea zawadi kutoka kwa wafanyabiashara.

Mahojiano hayo yaliyodumu kwa saa tatu, yalifanyika katika makao rasmi ya Netanyahu mjini hapa, baada ya mwendesha mashtaka mkuu wa Serikali kuanzisha uchunguzi wa kihalifu dhidi yake.

Vyombo vya habari nchini hapa vilisema uchunguzi huo unahusu zawadi zenye thamani ya mamia ya maelfu ya shekel (sarafu inayotumiwa nchini humo).

Netanyahu na mke wake Sara wamekwishanusurika kashfa kadhaa siku za nyuma, ikiwamo madai ya matumizi mabaya ya fedha za umma, na ukaguzi wa mahesabu juu ya matumizi ya familia yao.

Kiongozi huyo alisema hajatenda kosa lolote kuhusu shutuma hizo mpya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles