25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

Benitez asisitiza kuibakisha Newcastle Ligi Kuu

Rafa BenitezLONDON, ENGLAND

BAADA ya klabu ya Newcastle kuchezea kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Leicester City, kocha mpya wa klabu hiyo, Rafa Benitez, amesisitiza kuibakisha timu hiyo katika michuano ya Ligi Kuu.

Klabu hiyo kwa sasa ipo katika wakati mgumu wa kushuka daraja, lakini kocha huyo ambaye ameanza kibarua chake mwanzoni mwa wiki hii, amedai bado timu hiyo ina nafasi ya kuendelea kuwa kwenye ligi.

Hata hivyo, mchambuzi wa masuala ya soka wa Sportsmail, Jamie Carragher, anaamini kocha huyo wa zamani wa klabu ya Liverpool, hana wachezaji wa kutosha kuweza kuibakisha klabu hiyo kwenye ligi.

“Kama hatupati ushindi nachukia, lakini nina furaha kuona wachezaji jinsi walivyojitoa kwa ajili ya timu yao japokuwa imefungwa.

“Hadi sasa nimegundua kitu cha kufanya ili kuweza kuibakisha timu kwenye ligi msimu ujao, kila mchezo uliopo mbele yetu ni muhimu sana ili kuhakikisha malengo yanatimia.

“Nimewaambia wachezaji wangu mchezo ujao dhidi ya Sunderland ni kama fainali, kila mchezaji anatakiwa kupambana, mashabiki nao ni kama wachezaji kwa kuwa wana mchango mkubwa katika ushindi,” alisema Benitez.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles