28.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 21, 2024

Contact us: [email protected]

Barcelona, Arsenal hapatoshi leo UEFA

afc_v_barca_ucl-696x372BARCELONA, HISPANIA

MICHUANO ya Klabu Bingwa barani Ulaya inatarajia kuendelea tena leo kwenye viwanja viwili, huku mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Barcelona watakuwa kwenye Uwanja wa Nou Camp wakipambana na Arsenal, wakati huo Bayern Munich wakiwa kwenye Uwanja wa Allianz Arena dhidi ya Juventus.

Mashabiki wa soka wanadai kwamba siku hii ya leo dunia itasimama kwa muda wa saa 1:30 kuipisha michezo hiyo ya wababe wa soka.

Kwa mchezo wa Barcelona, wapo wadau wa soka ambao wanasema kwamba kazi ni nyepesi kwa mabingwa hao watetezi kuingia hatua ya robo fainali kutokana na kile ambacho walikifanya kwenye Uwanja wa Emirates ambako wenyeji Arsenal walipokea kichapo cha mabao 2-0.

Katika mchezo wa leo, Barcelona inahitaji ushindi au sare ya aina yoyote kuweza kuingia hatua hiyo, wakati huo Arsenal wanahitaji ushindi kuanzia mabao 3-0 na inaonekana kuwa kazi kubwa kuweza kuizuia safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo ambayo inaongozwa na Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar wasiweze kupata bao hata moja.

Baada ya kumalizika kwa mchezo wa awali kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, alisema kwamba Barcelona wana nafasi kubwa ya kuingia hatua ya robo fainali kutokana na ubora wao.

Mchezo mwingine ambao unatarajiwa kuangaliwa na watu wengi ni kati ya Mabingwa wa Ligi Kuu nchini Ujerumani, Bayern Munich dhidi ya wapinzani wao, Juventus.

Huu ni mchezo wa kuoneshana ufundi na kutumia nafasi kwa umakini wa hali ya juu, mbali ya wachezaji, hata makocha tunatarajia kuona makubwa kutoka kwao kwa kuwa kila timu ina wachezaji wazuri na ni bora, lakini timu moja lazima iyaage mashindano hayo.

Mchezo wa awali timu hizo zilitoka sare ya 2-2, hivyo mchezo wa leo atakayefungwa atayaaga mashindano na haitabiriki nani anaweza kushinda kwa kuwa soka ni mchezo wa makosa, ila tunatarajia kuona soka la hali ya juu na ushindani mkubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles