27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

FA kumfungia Diego Costa

Diego CostaLONDON, ENGLAND

CHAMA cha Soka nchini England (FA), kinatarajia kumsimamisha mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa, kutokana na kitendo cha utovu wa nidhamu ambacho alikionesha kwenye mchezo dhidi ya Everton mwishoni mwa wiki.

Hata hivyo, mchezaji huyo alioneshwa kadi nyekundu katika mchezo huo, lakini FA imesema kwamba japokuwa mchezaji huyo alioneshwa kadi nyekundu bado kuna uwezekano wa kufungiwa michezo mingine kutokana na utovu wa nidhamu aliouonesha.

Katika mchezo huo wa Kombe la FA, Chelsea ilikubali kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Everton na kutolewa katika hatua hiyo ya robo fainali.

Ilidaiwa kwamba, Costa alimng’ata mchezaji wa Everton, Gareth Barry, lakini mshambuliaji huyo wa Chelsea alikanusha kufanya kitendo hicho, hivyo FA inaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo.

Januari 27 mwaka jana, mchezaji huyo aliwahi kusimamishwa michezo mitatu kutokana na utovu wa nidhamu ambao aliuonesha kwenye mchezo dhidi ya Liverpool, baada ya kumchezea vibaya Emre Can, katika mchezo wa Capital One hatua ya nusu fainali.

Septemba 19, alisimamishwa michezo mitatu baada ya kumshambulia mchezaji wa Arsenal, Laurent Koscielny usoni, wakati huo Januari 7 mwaka huu ilidaiwa kugombana na mchezaji mwenzake, Oscar wakati wa mazoezi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles