23.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Ben Pol kuwafanyia ‘surprise’ mashabiki Januari

ben pzyyyyyNA KHABIB NASSORO (MUC)

MSANII wa muziki wa  RnB nchini, Benald Paul ‘Ben Pol’, amepanga kuwafanyia ‘surprise’ mashabiki wake mwanzoni mwa mwaka 2016 kwa wimbo mpya alioufanya na msanii mkubwa kutoka Afrika Mashariki.

Akizungumza na MTANZANIA jana, mwanamuziki huyo alisema amemaliza mwaka kwa wimbo mpya na atafungua mwaka kwa wimbo mpya.

“Nimefunga mwaka kwa kuachia video yangu mpya ambayo inajulikana kwa jina la ‘Ningefanyaje’ huku nikishirikiana na Avril kutoka Kenya, ila nitafungua mwaka kwa wimbo mpya ambao sitapenda kuutaja jina mapema, lakini nimefanya na msanii toka nje ya Tanzania na itakuwa ni ‘surprise’ kwa mashabiki wangu,” alisema Ben Pol.

Msanii huyo aliongeza kwa kusema kwamba, mwaka 2016 utakuwa wa mafanikio makubwa kwake kutokana na jinsi alivyojipanga na ushindani uliopo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles