24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

Bella kutikisa Dar Live kesho

BellaNa Mwandishi Wetu

MKALI wa sauti, Christian Bella, anatarajiwa kupagawisha mashabiki wake kesho kwenye ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

Msanii huyo anatarajia kushuka jukwaani na wimbo mpya ambao anatamba nao kwa sasa alioufanya na mkongwe wa muziki kutoka Kongo (DRC), Koffi Olomide, uitwao Acha Kabisa.

Mkali huyo mwenye kibao cha ‘Nashindwa’ anatarajia kufunga mwaka kwa kukata kiu kwa mashabiki wake kwa kuimba na kucheza ngoma zake zote kali kama vile Nani Kama Mama, Nakuhitaji, Msaliti, Nashindwa, Amerudi na nyingine kibao.

Mashabiki pia wategemee kupata sebene la aina yake kutoka kwa Malaika huku kukiwa na wakali kama Adaya, Petit Mauzo, Pilu, Mico Bella, Chesco Vuvuzela, Yanick Soslo, Babu Bomba, Kadogoo Machine na wengine wengine wengi.

Baada ya kufunga mwaka, katika Sikukuu ya Mwaka Mpya (Januari 1), bendi kongwe ya muziki wa Dansi, The African Stars ‘Twanga Pepeta’ ikiongozwa na Ali Chocky itakuwa na kazi moja ya kulishambulia jukwaa kwa kutoa sebene la kisasa kwenye ukumbi huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles