Ben Pol ajipanga kwa albamu mwaka huu

0
716

Ben PaulNA THERESIA GASPER

MSANII wa Bongo Fleva, Benard Paul ‘Ben Pol’ yupo mbioni kuachia albamu yake itakayokuwa na nyimbo 12 kwa mwaka huu.

Ben Pol alisema yupo katika hatua za mwisho za kukamilisha albamu hiyo kama alivyopanga huku uzinduzi wake ukitafutiwa siku maalumu ya kuutangaza.

“Nikishakamilisha kila kitu ndio nitaweka wazi inatoka lini pamoja na jina lake na namna ya uzinduzi kama utakuwepo ama la,” alisema Ben Pol.

Alisema kwa sasa yupo kwenye hatua za mwisho kukamilisha suala hilo huku akiwa anapanga kuwapa ladha tofauti  wapenzi wa muziki wake.

“Kabla ya albamu yangu hii nitaachia nyimbo mbili nyingine kwa mashabiki wangu hivi karibuni.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here