24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

BELLE 9 AFUNGA NDOA KIMYA KIMYA

NA MWANDISHI WETU


BAADA ya picha za harusi za msanii wa Bongo fleva, Abelnego Damian ‘Belle 9’ kusambaa mitandaoni, mkali huyo amefunguka na kusema ni kweli na asilimia kubwa ya matukio kwenye muziki wake ni maisha yake halisi.

Akizungumza na MTANZANIA, Belle 9 alisema amekuwa akifanya mambo kwa kujiamini, licha ya watu kudhani ni kiki, lakini ni kweli amefunga ndoa mkoani Morogoro.

“Watu wanadhani ni ujio wa wimbo wangu, watambue muziki wangu unajitosheleza bila kiki, nilioa tarehe 16  siku ya Jumamosi mkoani Morogoro na nimeamua kufanyia huko kwa sababu familia yangu yote ipo huko,” alisema Belle 9.

Alisema amekuwa akipenda maisha ya usiri na ndiyo maana watu wengi wameshindwa kuamini kama ni kweli picha zile ni halisi au wimbo.

Alisema kuwa, anampenda sana mke wake na wamekubaliana kuishi pamoja kwa kuwa kila mmoja ameridhika na mwenzake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles