ALIYEBEBA MIMBA YA KIM, KANYE AANIKWA

0
739

LOS ANGELES, MAREKANI


HATIMAYE nyota wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Kanye West na mke wake, Kim Kardashian, mwanzoni mwa wiki hii wameonekana wakiwa na msichana aliyebeba mimba yao.

Wawili hao mapema mwakani wanatarajia kupata mtoto wa tatu kwa njia ya kupandikiza, hivyo mapema wiki hii walionekana mtaani wakiwa na msichana huyo ambaye amepandikizwa ujauzito wa wawili hao.

Kim na Kanye wameweka wazi kuwa, watakuwa eneo la tukio wakati msichana huyo akiwa anajifungua ili kumshuhudia mtoto wao.

Kupitia akaunti yao ya Instagram, wawili hao wamedai wana furaha kubwa kuona kwamba wanatarajia kuongeza ukubwa wa familia mapema mwakani.

“Muda unakaribia, tunaamini ndoto zetu zinakaribia kutimia, furaha yetu ni kuona familia hii ikiendelea kuwa kubwa,” waliandika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here