22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Bei ya mbolea yashuka kwa asilimia sita

Nora Damian

Mfumo wa Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja (BPS), unaotumiwa kuagiza mbolea ya kupandia (DAP) na ya kukuzia (Urea) umerahisisha kupunguza bei ya mbolea kwa kati ya asilimia 6 – 17.

Mfumo huo ulianzishwa na Serikali mwaka 2017 kwa lengo la kupata punguzo la bei litokanalo na kununua na kusafirisha mbolea nyingi kwa wakati mmoja.

Akizungumza leo Jumatano Agosti 28, wakati wa kutangaza bei elekezi ya mbolea ya kupandia kwa msimu wa kilimo wa 2019/20, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, amesema uanzishwaji wa mfumo huo sambamba na kufuta tozo mbalimbali ni mojawapo ya utekelezaji wa Azimio la Abuja la mwaka 2006.

“Tumeendelea kuhamasisha matumizi ya mbolea ili kufikia kilo 50 za virutubisho kwa hekta moja kama ilivyopendekezwa na Azimio la Abuja. BPS kwa sasa inatumika kuingiza mbolea za DAP na Urea ambazo ni takribani asilimia 50 ya mbolea zote zinazotumika nchini,” amesema Hasunga.

Amesema kulinganisha na msimu uliopita bei ya mbolea kwa kilo 50 imeshuka kutoka Sh 67,103 (2018/19) hadi Sh 58,419 (2019/20), wakati kwa kilo 25 imeshuka kutoka Sh 35,552 hadi Sh 30,209 na kwa kilo tano bei imeshuka kutoka Sh 7,910 hadi Sh 6,642.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles