27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Bavicha wakwama Polisi

NAPENa Veronica Romwald

JESHI la Polisi limesema haliyatambui maandamano yaliyopangwa kufanyika kesho na Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha).

Maandamano hayo ya kuelekea Ikulu yanalenga kufikisha ujumbe kwa Rais John Magufuli wa kupinga uamuzi wa Serikali uliotangazwa bungeni na Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, unaoitaka Televisheni ya Taifa (TBC) kusitisha kurusha hewani vikao vya Bunge.

Akitangaza uamuzi huo, Waziri Nape alisema umefikiwa baada ya kubaini gharama za kurusha matangazo hayo ni kubwa na kwamba wafanyakazi wengi wamekuwa hawatimizi majukumu yao ipasavyo kutokana na kufuatilia vikao hivyo.

Akizungumzia msimamo wa polisi, Afande Sirro alisema hajapata uthibitisho wa kupokelewa kwa barua ya kufanyika maandamano hayo na Ikulu hivyo hayatambuliki.

“Walituletea hiyo nakala ya barua waliyoipeleka Ikulu, lakini hata yenyewe haikuwa inaeleza kwamba wameruhusiwa kwenda, hivyo sisi tunasimamia msimamo ule wa Serikali wa kutoyatambua maandamano hayo.

“Kama wanataka kuwasilisha hoja yao kuhusu vipindi vya moja kwa moja vya Bunge kupitia Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), ni vema wakatumia njia nyingine, lakini si ya maandamano, kwani tumebaini kwamba kuna viashiria vya uvunjifu wa amani,” alisema Afande Sirro.

Wiki iliyopita Katibu Mwenezi wa Bavicha, Edward Simbeya, alitangaza kupinga uamuzi wa Serikali uliotangazwa na Nape kuzuia kurushwa matangazo ya Bunge moja kwa moja na TBC, akidai kuwa ni ya kidikteta yaliyolenga kuwanyima haki Watanzania kuona kazi zinazofanywa na wawakilishi wao bungeni.

Alisema Bavicha itaandamana kwenda Ikulu kufikisha ujumbe wa Rais Magufuli ili atengue uamuzi huo.

Maandamano hayo ambayo awali yalipangwa kufanyika siku ya Jumatatu, yalikwama baada ya Afande Sirro kueleza kuwa yalipangwa kufanyika siku ya kazi, hivyo yangeweza kusababisha vurugu na kusimamisha baadhi ya shughuli za wananchi.

Aidha, Kamanda Sirro pia alisema maandamano hayo hayawezi kupewa kibali kwa sababu Ikulu haina taarifa rasmi za ugeni wa vijana hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles