28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Basi lagonga treni Dar, mmoja afariki dunia

Salum Hamduni
Salum Hamduni

Na ASIFIWE GEORGE, DAR ES SALAAM

MTU mmoja amefariki dunia na wengine 43 wamejeruhiwa katika ajali ya treni iliyotokea eneo la Kamata Kariakoo, Dar es Salaam juzi usiku.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Ilala, Salum Hamduni, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 4:00 usiku wakati treni hiyo ikitokea Stesheni kwenda Ubungo.

Alisema treni hiyo ilipofika katika Kituo cha Kamata Kariakoo, basi namba T 696 CVB mali ya Kampuni ya UDA liliigonga na kusababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi hao.

“Dereva wa basi hilo alisimamishwa na mtu aliyekuwa akitoa ishara kwamba asipite kwa sababu treni ilikuwa karibu, lakini alikiuka agizo hilo na kupita, ndipo ajali hiyo ikatokea.

“Tunaendelea kumshikilia dereva wa basi hilo kwa   mahojiano na upelelezi ukikamilika hatua za  kisheria zitachukuliwa dhidi yake, ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani,” alisema Kamanda Hamduni.

Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na majeruhi wanaendelea kutibiwa hospitalini hapo.

Kamanda Hamduni aliwataka madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani, kuepuka matatizo kama hayo ambayo yanasababishwa na uzembe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles