26.7 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Bashe: Sheria zinazokinzana na kasi ya Magufuli zifutwe

Pg 16Na Khamis Mkotya, Dodoma

HOTUBA ya Rais Dk. John Magufuli, imeendelea kujadaliwa bungeni, huku baadhi ya wabunge wakionekana kufurahishwa na kasi ya utendaji wa kiongozi huyo katika kipindi kifupi alichokaa Ikulu.

Akichangia hoja hiyo bungeni jana, Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM), aliishauri Serikali kuwasilisha bungeni sheria zote zinazokinzana na kasi ya Dk. Magufuli ili ziweze kufanyiwa marekebisho.

Bashe alisema yapo malalamiko mbalimbali kuwa kasi ya rais inayofanyika hivi sasa imekuwa ikikinzana na baadhi ya sheria za nchi.

Mbunge huyo alisema baadhi ya sheria zilizopo hivi sasa zimekuwa ni kichaka kikubwa cha wezi wanaoliibia taifa.

Akitoa mifano, aliitaja Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2004 kuwa ni kati ya sheria zinazohitaji kurekebishwa, kwani imekuwa ikitoa mwanya kwa watumishi wa Serikali kuliibia taifa.

“Utaona kwa kutumia sheria hiyo, tundu la choo linajengwa kwa Sh milioni 20, kupitia wakandarasi wao, wakati choo hicho hata milioni tano hazifiki,’’ alisema.

Kwa mujibu wa mbunge huyo, kunahitajika kiongozi kama Dk. Magufuli katika kufanya uamuzi sahihi ili jamii iweze kuondoka hapa ilipo na kupiga hatua.

“Watu wanahoji eti kwanini Serikali imetoa fedha na kupeleka shuleni bila kupitia bajeti ndogo, sasa ulitaka watoto wetu wasiende shule,’’ alisema.

Bashe alisema hotuba hiyo ya rais aliyoitoa bungeni imetoa taswira kuwa Dk. Magufuli ndiye rais ambaye Watanzania walikuwa wakimhitaji kwa ajili ya mageuzi nchini.

Aidha mbunge huyo aliiomba Wizara ya Fedha kuhakikisha inatenga fedha za kutosha kwa ajili ya ujenzi wa reli kwa ukubwa wa ‘standard gauge’.

Alisema reli ni njia muhimu ya kusafirisha mizigo mbalimbali ikiwamo hata ya nje ya nchi.

“Tumeona ‘political will’ (utashi wa kisiasa) ya rais kuifanya nchi kuwa ya viwanda, lakini yako mengi tunapaswa kuyafanya kama wabunge.

 

KIKWEMBE

Naye Mbunge wa Kavuu, Dk. Pudensiana Kikwembe (CCM), akichangia hotuba hiyo alisema suala la elimu bure ni muhimu likatolewa ufafanuzi zaidi kwa sasa.

Alisema kumekuwa na sintofahamu miongoni mwa watendaji wanaotekeleza sera hiyo kwani bado kuna changamoto nyingi.

“Nawaomba walimu wakuu kutumia fedha hizo kwa lengo lililokusudiwa na si vinginevyo,” alisema.

 

MASELE

Mbunge wa Mbogwe, Agustine Masele (CCM), aliwataka Watanzania kumwombea Rais Magufuli kwa kazi nzito anayoifanya ya kutumbua majipu.

Alisema hivi sasa taswira ya nchi imeanza kuonekana kutokana na majipu kutumbuliwa kila kukicha.

Akizungumzia viwanda, mbunge huyo alisema ni muhimu vikafufuliwa ili kuongeza ajira kwa wananchi walio wengi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles