29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Basata yaanzisha mfumo mpya

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata) limeanzisha kanzidata ‘database’ ya kuhifadhi kumbukumbu na taarifa mbalimbali za kumbi za starehe na burudani nchini ili kurahisisha upatikanaji wa takwimu sahihi katika sekta ya sanaa.
Akizungumza jijini hivi karibuni wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili ya watendaji wa Basata kuhusu matumizi sahihi ya kanzidata, Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Godfrey Mngereza alisema wanaimani malengo ya kuhifadhi taarifa na takwimu zote zihusuzo sekta ya sanaa yatatimia.
“Tumeanza na kumbi za starehe na burudani zilizoko nchi nzima, lakini lengo ni kuweza kuhifadhi taarifa za wasanii wote nchini, mapromota, vyama vya wasanii na asasi mbalimbali zilizosajiliwa,” alisema Mngereza.
Alisema Basata imedhamiria kuhama mfumo wa kianalojia na kuanza kuhifadhi nyaraka na taarifa zake kidijitali, ambapo programu hiyo ya kanzidata itafanyika kwa awamu hadi itakapokamilika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles